Ume
Shikamoo kwa Mume kutoka kwa mkewe inategemea na asili ya familia na mahusiano baina ya mke na mume bila kujali umri. Mfano:
1. Mke humuamkia mume mbele ya watoto ili kujenga kwa watoto kuwa baba ni kichwa cha nyumba na watoto hupokea hilo maishani mwao. Lakini wazazi wanaweza kuwajenga pia watoto wao katika salamu za kiimani kwa hivyo shikamoo sio lazima.
2. Kuna shikamoo ya mahaba ambayo mke huwa anampa mumewe. Narudia hii huwa ni shikamoo ya mahaba na utani wa kimapenzi yaani mke na mume huwa katika hali hiyo nyakati fulani fulani si mara zote ( hili hutokea automatic kwa mke wangu mara chache sana hasa nikirudi nikiuliza hujambo mke wangu nae hujibu kwa kusema "sijambo mume wangu shikamoo" na wote huwa tunaishia kucheka. Jambo hilo hutokea kwa mwaka mara moja au mara mbili. Mke wangu ni age mate wangu kabisa.
3. Shikamoo ikitumika visivyo itajenga distance kati ya mke na mume. Hasa kwenye familia yenye migongano kwa wingi na mawasiliano hafifu.
NB: shikamoo, salamu inayoweza kukubaliwa na wanandoa husika kuwa sehemu ya maisha yao au kutokea mara chache kama ajali. Au isitokee kabisa lakini maisha yakasonga. Kikubwa kila mwanandoa awajibike kwa nafasi yake hapo ndipo heshima ya kweli hutokea. Hasa baba kutoa mitonyo ya kulea familia.
Umeeleza vizuri sana ila mkuu rafiki yangu she is 30 anatoka na mbaba 55yrs (mchepuko) ina maana huyu baba alimjua shoga yangu kupitia mimi coz huyu baba tunafanya kazi sehem.moja.
Mimi huyu baba namsalimia kabisa shikamo kubwaaaa tu. Rafiki yangu kabla hawaja date alikuwa akimsalimia shikamooo sasa hivi wanadate anahisi kuendrkeza shikamoo ni kuweka gap kama ulivyo sema.
Huyu baba ili kulinda ndoa yake ana mu adress shoga yangu kama 'dada' ambayo alikuwa akimuita kabla ya kudate.
Wanadate kwa siri sana( mbaba huyu atakiwi kujulikana kitokana na status).
Shoga tukiwa kwenye umbea ndo ananiuliza je shikamoo iendelee au?
Huyu mbaba akimpigia simu hata wewe ukiwa karubu huwezi hisi kama wanadate.
Mfano akipiga simu:
Mbaba: mambo dada? Hujambo dada?
Shoga yangu: sijambo shikamoo😅.......hapa sasa ndo tunacheka hatuna mbavu......mara dada lakini niwapenzi wa siri sana.
Shoga ananiuliza akiendelea kumsalimia si ndo anaendelea kumuwekea hayo ma status yake?
Nilimuuliza shoga mkiwa faraga mnaitanaje? Akasema hatuitani majina yoyote wanakula wanacheka basi hivyo na anamuhudumia.
Tatizo la huyu mbaba rafiki yangu ni mpole sana ana maneno machache ila mcheshi.
Siku moja nikamtania ' vip nimekupa kitu chenya TBS? akajibu "super" hapo kamaliza
Mimi naona huyu akiendelea kusalimiwa mmh shoga kazi anayo.