SHILAWADU bana,leo kipindi kizima stori za Diamond

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,577
Reaction score
3,146
Naangalia hawa madogo,naona leo ni stori za diamond tu karibia lisaaa lizima,huku wakimpiga vijembe Sallam eti awaachie msanii wao...kumbe wanampenda sana Chibu na wananjua kabisa bila chibu kipindi chao hamna kitu...hii ni ishara clouds media bila diamond haina mvuto!!!
 
Soma alama za nyakati,hiyo ni starting point ya kuanza kucheza nyimbo za WCB km umeona,wamepiga ngoma ya Ntakufilisi ya Darlin na na wanapiga stor za Darlin na dingi ake....clouds na Diamond ni kitu kimoja hao kugombana hawawezi.
 
Eti wanajaribu DIVIDE AND RULE


SI WALIJIDAI WANAMFUNGULIA ASLAY DUNIA HAWA,DOGO ETI ANAONEWA WIVU,imekuaje tenaaaa waseme waachiwe msanii wao,wameona nguvu ya UMMA nyuma nn
 
Ukimiliki chombo cha habari, unaweza kugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli na mtu pekee aliyeweza kumkomesha ruge ni Zamaradi sababu tu alikuwa na tangible evidence ya sauti na ndio maana shilawadu walivyoposti habari za kumkandamiza na yy nae akalipua bomb kwa kuachia sauti, la sivyo tungejua mpaka chupi ya Zamaradi zina rangi gani, zinamatundu mangapi, baadaye soudybrown akafuta ile post inayomuhusu Zamaradi. Ila namuomea huruma Diamond platnumz, kila mtu anajifanya mshauri ili kutetea maslai yake, kama kweli wao wanaweza kumbeba msanii mbona wameshindwa kwa Barnaba (msanii PEKEE aliyekamilika kwa kila kitu), lkn leo barnaba ukimtizama anatia huruma. Kweli more money, more haters, ila ruge anajua kuwatumia akina Soudybrown (hamna mwanahabari huru mbele ya bosi wake).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…