Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SHILINGI BILIONI 2.6 ZATENGWA KWAAJILI YA MATENGENEZO YA BARABARA JIMBO LA MBOGWE
"Ili kukarabati Barabara katika Jimbo la Mbogwe, kiasi cha Shilingi Bilioni 2.6 zimetengwa katika mwaka 2024/2025 kwaajili ya kuendelea kutengeneza matengenezo ya Barabara. Fedha zilizotengwa zitatumika pia kwaajili ya kujenga Barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Mita 700 ambapo Shilingi Milioni 570 zimetengwa.
Aidha, Shilingi Bilioni 1.82 zimetengwa kwaajili ya kujenga Barabara kwa kiwango cha Changarawe yenye urefu wa Kilomita 111.14 na Shilingi Milioni 241 zimepangwa kwaajili ya kuweka Makarvati 50 katika maeneo mbalimbali kwa upana wa Barabara wa Mita 7.
Katika mwaka 2023/2024 yamefanyika matengenezo ya Barabara kwa kiwango cha Changarawe kwa jumla ya urefu wa Kilomita 142.7 na Barabara za Udongo Kilomita 14.2 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 2.688 na Makarvati mistari 60 kwa gharama ya Shilingi Milioni 360.7
Serikali itaendelea kuhudumia miundombinu ya Barabara za Wilaya ya Mbogwe kwa Kuzijenga, Kuzikarabati na Kuzifanyia matengenezo kulingana na upatikanaji wa fedha" - Amesema Mhe. Zainab Athuman Katimba, Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI
"Serikali ilijenga Barabara za Lami Mji wa Masumbwe (KM5), Lini sasa itaweka Taa za Barabarani? Makao Makuu Halmashauri ya Mbogwe ilishaomba KM 2 za Lami. Ni lini Serikali itatupa fedha ili Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ipate lami? - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe