Shilingi Bilioni 891.5 za Rais Samia zilivyotumika mtaa kwa mtaa

Shilingi Bilioni 891.5 za Rais Samia zilivyotumika mtaa kwa mtaa

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezungumzia mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita, amezungumza akiwa katika Ofisi za Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), leo Machi 4, 2022.

Haya hapa ni baadhi ya mambo muhimu ambayo ameyazungumza ambayo yamekuwa na faida kubwa kwa raia wa kawaida.

#Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kikubwa katika Sekta ya Afya kipindi cha mwaka mmoja tangu kuingia madarakani ambapo jumla ya shilingi Bilioni 891.5 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Wizara ya Afya.

# Miradi ya maendeleo ya kipaumbele iliyotekelezwa moja kwa moja na Wizara ya Afya ni pamoja na;

# Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za afya katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Rufaa za Kanda, Hospitali Maalumu na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kiasi cha shilingi bilioni 90.4 zilitolewa.

# Ukarabati wa majengo ya kufundishia katika Vituo vya Afya ambapo kiasi cha shilingi bilioni 6.3 kimetolewa. Ununuzi na usambazaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, ambapo jumla ya shilingi Bil. 333 zimetolewa.

# Kununua Vifaa Tiba vya Uchunguzi, kuimarisha huduma za upatikanaji wa damu salama.

# Kugharamia posho za wanafunzi watarajali (Intens) wa Udaktari, Udaktari wa Meno na wataalam wa Afya Shirikishi kiasi cha shilingi Bil. 49.9 zimetolewa.

# Kulipia gharama za masomo kwa ajili ya Madaktari bingwa (specialists) na Madaktari bingwa Bobezi (Super Specialists) ndani na nje ya nchi ambapo jumla ya shilingi Bil. 4.4 zimetolewa.

# Kuimarisha mapambano dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (ikiwemo ununuzi wa dawa ARVs, Dawa za Malaria na Vitendanishi) ambapo kiasi cha shilingi bilioni 117 kimetolewa.

MATOKEO YALIYOPATIKANA
# Kuboreshwa kwa miundombinu ya kutolea Huduma za Afya.

# Kuimarika kwa Upatikanaji wa Huduma za Matibabu ya Ubingwa Bobezi (Super specialized) nchini.

#Kuimarika upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa Tiba, vitendanishi katika vituo vya umma vya kutolea huduma za afya.

#Kuimarika kwa Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.

#Kuendelea kupunguza Idadi ya Wagonjwa na Vifo vinavyotokana na UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu (TB)...

FM_D0W2XoAE8KVq.jpg
 
Kongole kwa serikali..ila kwa staili hii ya matumizi ya pesa kwenye sekta ya afya sio leo wala kesho kupambana na adui maradhi.

Ukijenga hospitali manake unatarajia au una wagonjwa wengi..

Ukiongeza bajeti ya madawa na vifaa tiba mana una wananchi wengi wagonjwa au unatarajia wagonjwa zaidi.

Kwa mtazamo huo tuna wizara ya wagonjwa na wala sio wizara ya afya.

Wizara ya afya inapaswa kujikita zaidi kwenye public health approaches dhidi ya magonjwa iwe ndio kipaumbele hususani masuala ya chanjo dhidi ya magonjwa..kuimarisha afya ya msingi..kwa kudhibiti magonjwa kupitia usambazaji wa maji safi na salama..matumizi ya vyoo bora..usimamizi wa mazingira kwa kuuwa mazalia ya mbu na wadudu waenezao magonjwa.

Kuimalisha afua za lishe..ubora na usalama wa chakula..utoaji wa elimu ya afya dhidi ya magonjwa..ushirikishwaji wa jamii katika masuala yote yahusuyo afya.

Tukumbuke kauli ya mwalimu JK Nyerere alisema "MTU NI AFYA"

Mtajenga mahospitali makubwa..mtaongeza bajeti za madawa kila mwaka..ila kama hamtoweza kuzisimamia na kuziimalisha public health approaches kamwe mzigo wa magonjwa hutaisha bali utaendelea kukuwa siku hadi siku.

Na bajeti mtatenga siku hadi siku mabilioni kwa mabilioni ila hamtaweza kuwa na wanachi wenye afya bali wagonjwa.

Kinga ni bora kuliko tiba..imalisheni kinga wakati ndio huu.

Acheni afya siasa kwenye afya za wananchi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom