Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SEKTA YA ELIMU KATIKA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI
Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, (Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara) tarehe 28, Mei, 2023 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mufindi iliyopo Kata ya Ikongosi.
Shule ya Sekondari Mufindi ina Madarasa Nane na ofisi Nne, pamoja na jengo la utawala (Administration Block), Chumba cha Kompyuta (Computer room/ICT), Maktaba, Matundu 20 (Wavulana Matundu 10 na Wasichana Matundu 10) ya Vyoo vya Kisasa na Maabara ya Kisasa ya Kemia, Fizikia na Biolojia.
Mradi wa Shule ya Sekondari Mufindi umetekelezwa kwa Jumla ya Tsh Milioni 550 ikiwa fedha kutoka Serikali Kuu, Halmashauri (W) Mufindi pamoja na Nguvu za Wananch.
Shule ya Sekondari Mufindi imefunguliwa na ina jumla ya Wanafunzi 171 wanaoendelea kupata Elimu.
Shukrani za dhati kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuwezesha Wana Mufindi Kaskazini kutekeleza Ilani ya CCM 2020-2025.
Aidha, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel hongolo katika ziara yake mkoani Iringa alipita kukagua Shule ya Sekondari Mufindi iliyopo Kata ya Ikongosi ambapo alikaribishwa na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mhe. Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe kuhutubia wananchi.
#Maendeleo ni Mchakato Endelevu, Maendeleo ni Watu.
Kazi Iendelee