Leo tumehabarishwa na Benki Kuu ya Tanzania(BOT) jinsi shillingi ya Tanzania bado ni HIMILIVU. Binafsi mimi sikuelewa maelezo yao lakini cha ajabu leo Dollar moja ya Kimarekeani ni Tshs.2,642.934 na wiki ijayo si ajabu utakuta Dollar moja ya Kimarekani itakuwa Tshs.3,000. Bado thamani ya shillingi yetu inashuka dhidi ya majirani zetu. Kwa mwendo huu kila kitu kitakuwa ghali hasa nishati ya mafuta. Gavana wa Benki Kuu unatakiwa kuchukua hatua za haraka.
