Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Hahaha aise
Ila ukipata shukuru

Ova
Hakuna mwanamke anampenda mwanaume asie na pesa , Hakuna mkuu. Mwanaume unaweza mpenda mwanamke na familia Yao nzima ni masikini lakini mwanamke hawezi kumpenda mwaume wa hivyo.


Na Kama ikitokea lazima Huyo mwaume ajiandae siku yoyote bomu litalipuka. Tumeyaona na nina Imani kwa umri wako umeyaona.
 
Hiyo ndo inaitwa mbwa kala mbwa...

We nenda kadange uniumize roho, nami nakuibukia usiku nakuumiza sura

Malipo ni hapahapa Duniani....

Mwisho wa siku kidumw kimeibuka na ushindi, Shilole kaomba poo
Uchebe mtata sana..
Yani anamtandika mwenzie akiwa kalala fofofo..halafu za uso.
 
We Uchebe hujui kwamba Neno la MUNGU linatutaka wanaume tuishi na wanawake kwa akili??. Unataka kuumuua mtia nia ya kugombea ubunge wa jimbo la IGUNGA
Hahahaa bado hajapewa ujumbe wa kamati kuu?maana ukishakuwa maarufu inzi wa kijani wanakuchukua!
 
Kwa hiyo kina Mo na wanaume wote waliomtete Shilole ni wajinga,, umeiona tweet ya Mo Dewji? Kwa hiyo nae ni mjinga.
Aliyekuambia kumpiga mwanamke ndio ubabe ni nani, huyo Uchebe kama mbabe kweli si angeenda kumpiga huyo mwanaume ambaye kwa mtazamo wake au mawazo yake anadhani ndio kikwazo

Grow up.. Being kind is not a weakness
Hao wakina Mo hatukuwaona kipindi Shishi anamtwanga Nuh Mziwanda na akawa anajitapa mitandaoni na clip zake zipo ingia kwa Millard Ayo uone. Huyo nuh Yuko tu kijitonyama ana stress za pombe kwasababu ya Huyo Shishi.


Sitetei mtu Kupigwa ila muwe mna balance mambo sio mwanaume anapigwa mnakula buyu ila Huyo Malaya akipigwa mnabinua midomo.
 
Kumekucha kumekucha mi nahisi shilole ndo anakosa, sasa kama kuna mdau hapo anasema shilole huwa analipiwa tiketi ya ndege anaenda mkoani kuna mchizi. Huko huwa anamtivua tope sijui ni ukweli maana wabongo sisi da 🙌
Yalimo Yamo!!!
Unaweza Kuona Watu Wameyapatia Kumbe.
Story Za Hawa Mnawaita Stars
Ndiyo Wanagongwa Tu Wakitafuta Maisha Nafuu
 
Sitetei kwa alicho kifanya Uchebe,Ila wanawake na hao wanaharakati vigeugeu,wakati dogo Nuhu Mziwanda alivyokuwa akitembezewa vitasa na Shilole mlimuona Shilole shujaa (SUPER WOMAN ) na Shilole alikuwa akijitapa mpaka kwenye Media.

Leo kakutana na mwenzake ngumi mkononi kabutuliwa mnadai ananyanyaswa.Hapo ndio utajua mwanamke anaye mpiga mwanaume mbele ya jamii huonekana SHUJAA na mwanaume anayempiga mwanamke mbele ya jamii honekana MNYANYASAJI.
 
Huwa nachukia sana nikiona mwanaume mwenzangu anapiga mwanamke. Hivi tunashindwa kuishi nao kwa akili?
Braza ayo maneno yaseme ukiwa pekeako... labda ushukuru unakutana na madem wa kawaida.... ila km kweli ww ni baharia lazima ushakutana na relationship kichef chef kweli kweli... solution yake huwa ndo hiyo tu..

Naeza kupa scenario inayopelekea umshushie kipigo.

Unaeza pata mtoto mzur umemuelewa(umeona maslahi yapo) af km kidume ukasema ishu ya tabia utamuweka sawa, siku zinakatika na yeye km kawaida anaonesha kakolea.... anapokuja kugundua we ni mstaarabu anaanza kuonesha hulka/vitabia vyake(vya ajab ajab ambavyo we huendani navyo) ss we ushakolea(una maslahi nae) na kukomaa kwamba atajirekebisha... pale ndo mambo yanabadilika... maana utashindwa kuvumilia.... na kabla hujakata shaur la kuachana nae lazma utakua umepambana nae sana kwa kumpa kichapo... tho kuna wengine huwa wanatulia na kuwa na tahadhar kwa kichapo(hasa akiona ana maslahi/kakuelewa).......
 
Officialshilole Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.

Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake. Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA

'Uchebe' ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.

Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.

Najua nitalaumiwa kwa kuweka hili mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO.. Nimefika mwisho, na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama alieamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake

Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike kuwakumbusha wanawake TUVUNJE UKIMYA, TUPINGE UKATILI, TUTAKUJA KUULIWA SABABU

Pia soma > Shilole amchapa makofi mpenzi wake Uchebe mbele za watu

Yani nguvu zte unamtime dem kalala ndo unampga kwl
 
Kwan unafikiri uchebe ni mariooo kwa shilole
Sema wanawake Wana maaudhi sana, ila siungi mkono kuwapiga ila wanakera sana na hawakumbukagi jema

Ova
Uvumilivu jamani..hakuna binadamu aliyemkamilifu..unaona uvumilivu unakishinda tafuta njia nyingine ya kumyoosha pasipo madhara...nakupa hongera kwa kutounga mkono hoja.
 
Ukiona mwanaume anampiga mwanamke ujue amekasirishwa kiasi ambacho hatamani tena kumwona huyo mwanamke. Mapenzi yanaumiza sana haswa wanaume ndio wanaoumia kupita kiasi kutokana na usaliti.

Sipendi kupiga mwanamke ila sishangai mtu akipiga mwanamke najua maumivu anayopitia na pia ndoa nyingi zinavurugwa na wanawake kuliko wanaume.

Unapooana wanaume wenye ndoa wanakesha baa wanakimbia mengi sana majumbani mwao. Halafu wanawake wanajifanya kama watakatifu sana wakati wengi ni mashetani wanaoishi duniani na kuvuruga sana wanaume
Excuses excuses
 
Back
Top Bottom