Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Officialshilole Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.

Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake. Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA

'Uchebe' ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.

Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.

Najua nitalaumiwa kwa kuweka hili mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO.. Nimefika mwisho, na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama alieamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake

Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike kuwakumbusha wanawake TUVUNJE UKIMYA, TUPINGE UKATILI, TUTAKUJA KUULIWA SABABU

Pia soma > Shilole amchapa makofi mpenzi wake Uchebe mbele za watu

I clicked on this,I'm a part of the problem...sorry guys!
 
Sio wanawake tu hata wanaume huambulia kipigo tena cha uhakika.Nenda kaoe mkoa wa Mara halafu jifanye wewe kidume una dharau uone
Labda wanichangie tena waanzie kumi kwa idadi na wanikute nimelewa bwi na wawe na silaha ila napo bado nitakahikisha natumia powerbank ya uanaume wangu kuwatoa at least 1 bila.....

Hivi unajua kitendo tu cha kuwa mwanaume tayari una goli moja ya ushindi.....?!
 
Sio swala la dharau Uchebe ata ukisikiliza interview zake ana sign zote za mwanaume mpigaji.

Controlling ya mke wake aonge na nani asiongee nani

He is short tempered ata utani wa babalevo kwenye nyimbo tu umemkera.

Anataka mke wake awe na tabia fulani

Shilole ukimsikiliza kwenye interview zake unaona ana muogopa sana mumewe anajihami na wanapokuwa pamoja ucheshi wake unapungus (ishara tosha kabisa kuna kitu akiko sawa nyuma ya pazia).

Binadamu yoyote mwenye tabia ya kupenda ku control maisha ya mwenzake ni tatizo; na akiwa mwanaume probability kubwa ni mpigaji wa makonde kama anapigana na mwanaume mwingine.

Uchebe looked abusive bila ata Shilole kusema.
 
Mwanamke wako akikukosea ukampiga mara mbili tatu hajabadilika wala kukuheshimu uyo mwache au jifanye tu mjinga kama huwezi kum control unless otherwise utapata kesi na vichomi buuure.
Hadi kupigana huko nasubiria nini, mimi akisha pandishiana na mimi tukafika ile point tunaangaliana usoni kwa hasira. Nitajifanya ugomvi umeisha ila ajue humo ndani hatolala tena..... Ata tafuta pa kwenda....
 
Tunayo shida katika jamii yetu. Nyie mabinti mkija kupata watoto kuweni sehemu ya suluhisho. Raise your sons properly...muwafundishe vizuri kuhusu mambo haya. Hali siyo nzuri

Ni kweli mkuu..ila unatulaumu wanawake bure,hili ni swala ni letu lote,watu hawajui tu kama mkizaa mnakua models kwa watoto wenu,mkiwa mnapigana kila siku mnacreate watoto wagomvi....so, ukiangalia familia zinazopitia magomvi..angalia wazazi wa huyo mtu aggressive utajua kuna tatizo mahali katika makuzi aliyekulia.....
 
Kama huna hela kumzidi mkeo huo ni uzembe wako sio wake.

Kama huwezi katafute masikini mwenzio.

Kama inakuuma sana wanawake kuwa na vipindi kwenye media, njoo tukuweke ndani na wewe utetewe kwenye media.

Sisi WANAUME hatutaki hivyo vipindi na hatupigi mwanamke.
 
Labda wanichangie tena waanzie kumi kwa idadi na wanikute nimelewa bwi na wawe na silaha ila napo bado nitakahikisha natumia powerbank ya uanaume wangu kuwatoa at least 1 bila.....

Hivi unajua kitendo tu cha kuwa mwanaume tayari una goli moja ya ushindi.....?!
Mwenzio huyo hapo kakiona cha mtema kuni

 
naona mnataka kuhalalisha vipigo ndani ya ndoa..
Ukiona mwanaume anajihami Sana ohh mke wangu ana kipato kikubwa..Mara mke wangu msomi..huyo hajiamini....! Wanaume wengi Sana hawajiamini!
Mwanaume ukijiamini automatic na Mke atakuheshimu tu iwe isiwe ..! Yaan piga ua..
Sasa wewe hata hela huna 😏 mawazo endelevu huna ..unashinda insta na fb dume Zima kuchek makalio...unalalamika daily..unalia Lia weee unajiweka nyuma tu lazima kikuume...
Wanawake popote mlipo fanyeni kazi kwa akili na heshimuni wanaume zenu...hawa watu wanatakaga tu heshima hata km hastahili...kitu kidg tu..mheshimu Ila wewe hakikisha akaunti inanenepa!
Wanaume mnaojiamini popote pale cheers🤸🏋️!
Pole Sana Shilole..
 
Unasemaje nenda kaoe wanawake wa kisii kenya ulete za kuleta uone mziki wake
Aaaaaah weee akikata hiyo kitu humo ndani nafungua bucha....aiseee familia yake watanisamehe tukio la ukatili nitakalomfanyia huyo takataka
 
Back
Top Bottom