Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

Huyu dada niliwahi kumuona airport ya Mwanza akiwa amelewa chakari na kuongea maneno ya ovyo ovyo..na yule jamaa kama sikosei alikua ndo mumewe baada ya siku kwenda nilipokuja kujua hata picha za huyo mumewe nilirudisha kumbukumbu nyuma ya kua alikua ni yeye siku ile akiwa na huyu Shilole kalewa,kwa nilicho kiona siku ile niliamini ni ngumu kuishi na mwanamke msanii au mwanamuziki yamkini. So kama amekula kichapo nadhani hajaonewa
Officialshilole Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.

Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake. Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA

'Uchebe' ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.

Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.

Najua nitalaumiwa kwa kuweka hili mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO.. Nimefika mwisho, na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama alieamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake

Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike kuwakumbusha wanawake TUVUNJE UKIMYA, TUPINGE UKATILI, TUTAKUJA KUULIWA SABABU

Pia soma > Shilole amchapa makofi mpenzi wake Uchebe mbele za watu

 
Mtu ni rahisi kuhoji kuwa unampigaje Mwanamke...lakini ukitengeneza picha Mwanamke akurudie usiku wa manane alafu ananuka pombe kama tank la Breweries..alafu ukimuuliza anaporomosha matusi...utafanyeje? utatoka nje umpishe uanze kulia?

Huyo Mama keshazoea Bw Wadogo aliokuwa anawamudu, wakimuuliza anawadunda...sasa hapo huenda alitaka kuendeleza mtindo wake akakutana na kisiki cha Mpingo..na hapo kajitokeza kupata huruma ya Watu kwa kuwa imekuwa kinyume na matarajio...kama yeye ndiye angekuwa anammudu jamaa kwa kipigo wala usingemsikia.

Kakutana na black belt.
 
Hivi kwanini uchebe anahukumiwa na jamii bila kusikilizwa ! nadhani kanuni za haki ya asili (natural justice )zinapaswa zituongoze na sio mihemuko na ushabiki.

Tusikilize pande zote then tufanye maamuzi, shilole huyuhuyu anayesema anapigwa sahizi ndiye huyuhuyu aliyekuwa anampiga Nuh Mziwanda...


Tusikilizeni utetezi wa pande zote
 
Nimepitia uzi huu kuanzia post ya #1 mpaka hii ya mwisho #576. Nilichogundua ni hiki:
• Ndoa NYINGI za waliomo humu zinamatatizo sana. Kuna watu wanapiga na kupiga wenzi wao.

• Katika familia nyingi za waliomo humu WANAWAKE wanavipato sawa au kuwazidi Wayne zao. Hii inapelekea u feminism wa hali ya juu katika mjadala huu.

• Wengi wa wanaume humu HAWANA kauli kwa wake zao ama ni kwa sababu ya UCHUMI wa mwanamke au status ya mwanamke aliojijengea nyumbani mwao.

• Wanaume wengi WANAMAUMIVU yao ambayo machozi ya maumivu hayo hudondokea tumboni. Wanatendewa ndivyo sivyo ma wenzi wao lakini HAWASEMI kwa hofu ya kuachwa ama kutengana!

• Wanawake wengi waliopitia na kuchangia uzi huu ni wanawake wa KIMJINI MJINI, maswala ya NDOA na NAFASI YA MWANAUME katika nyumba hawaithamini zaidi wanithamini pale gu Mumewe akiwa na UCHUMI imara.


• Mwisho ni dhahiri shahiri kwamba mbali na swala la SIASA NA DEMOKRASIA tuliofeli kama taifa, swala linalofatia kea kupata alama za juu kabisa tuliofeli kama taifa ni swala la FAMILIA na Mahusiano ndani ya Ndoa. Katika haya mawili tunatuzo ya NOBEL kwa kushindwa katika maeneo hayo.
 
Kiukweli mimi binafsi naona watu wote wanaokuja juu na kumtupia lawama Uchebe hawajui walitendalo.

Kwanza kabla ya kuropoka watambue ile ni ndoa, na ndoa ina mipaka yake na misingi yake, watu hawatakiwi kuanza kuongea eti apelekwe polisi kina baba Levo wanajiropokea tu.

Suala la ndoa na maamuzi ya ndoa ni ya watu wawili tu mwanamke na mwanaume so kuhusu Uchebe afanywe nini ilo ni suala la Shilole mwenyewe kama atalipeleka kwenye vyombo vya sheria au kwenye familia.

Pia huwezi jua Shilole kakosea nini na baada ya kufanya kosa alipo ambiwa alifanya nini huenda Shilole na yeye alirusha ngumi.

Pia wanawake ambao wanajua kabisa wao ndio kila kitu kwenye familia hua wanadharau sana wanaume wao.

Unakuta midume inashupalia Uchebe kumpiga Shilole wakati Shilole alipokuwa anampiga Nuhu Mziwanda ilikua kimya.
 
Aisee! Hivi mwanaume uliyekamilika unapataje nguvu za kumpiga mtoto wa kike namna hii???
Kumpiga mwanamke ni noma sana.

Kwanza kabisa, ni kuonesha kukosa control juu ya hisia zako mwanamme.

Pili, umeshindwa kumdhibiti huyo mwanamke asifanye mambo ya kukukasirisha. Inaonekana mwanamme huna ushawishi ndani ya nyumba. Unatumia nguvu badala ya ushawishi.

Tatu, hata ukijisema wewe mwamba barubaru. Mwamba barubaru anatakiwa ajijue yeye kama mwanamme kupigana atafute mwamba barubaru mwenzake mwanamme. Siyo ampige mwanamke. Hata kwenye riadha na michezo mingine wanawake wana ligi zao tofauti na wanaume.

Nne, unampiga mwanamke, ukimuharibu sura au mwili halafu mkapatana hasara mmekula wote.

Tano, kumpiga mwanamke maana yake wewe mwanamme umekosea kuchagua mwanamke wa kukaa naye. Ungechagua vizuri mngekosana ndiyo,lakini si kufikia kumpiga. Hivyo umejionesha hujui kuchagua mwanamke bora wa kuishi naye.

Kwa leo niishie hapa.

Hizi sababu tano zitishe kunfanya baharia yeyote ajitathmini kabla ya kumpiga mwanamke.

Kuna tano nyingine za ziada, lakini kwa leo niishie hapa.
 
Hata kama ni halali kumpiga mke akikosea ila sio kwa ukubwa ule wa kipigo. Tena kapiga sana usoni alidhamiria kumuumiza na hata wakiachana awe hana soko tena maana front Ofice kashaiharibu.
 
Kioo cha jamii lakini hakijulikani kama ni Concave au Convex [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
HUWA NAWASHANGAAA SANA WASANII WA KIBONGO, ETI MIMI NI KIOO CHA JAMIII[emoji28][emoji28]

ova
 
HUWA NAWASHANGAAA SANA WASANII WA KIBONGO, ETI MIMI NI KIOO CHA JAMIII[emoji28][emoji28]

ova
Kioo cha jamii wakati kila siku wenyewe wanajitazama kwenye kioo, bora hata wajiite vioo wa maBen10 [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Back
Top Bottom