Shilole avishwa pete ya uchumba, ndoa ya tatu yanukia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Msanii na mfanyabiashara maarufu, Zuwena Mohammed, anayefahamika kwa jina la kisanii Shilole, amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake mpya usiku wa kuamkia leo, Desemba 23,2024

Tukio hilo lilifanyika katika hafla ya kifahari ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa katika eneo la Kijitonyama, Dar es Salaam.

Iwapo Shilole ataamua kufunga ndoa, hii itakuwa ndoa yake ya tatu, baada ya ndoa zake mbili za awali kuvunjika. Ndoa yake ya pili ilivunjika rasmi Juni 2024, takribani miezi sita iliyopita.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu wa karibu, huku Shilole akionekana mwenye furaha tele, ishara kwamba amepata ukurasa mpya wa furaha maishani. Mashabiki wake wanatarajia mengi kutoka kwa msanii huyo, ambaye pia ni mmiliki wa migahawa maarufu ya Shishi Food.
Your browser is not able to display this video.
 
Bado ndoa nyingine mbili...
 
Mwaka 2020 ilikua kidogo niichukue hii mali kabla yayule mpiga picha, kuna michezo alinileteaga hakuweza kuweka sawa mapema nikamtupa mazima. Anapenda sana vijana wadogo hata kama yupo kwenye ndoam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…