Shilole najua utapita kwenye huu Uzi nataka nikuume sikio.Kabla ya yote nikwambie tu hizi picha zisikuffishe moyo najua hiyo tabia mbaya umeshaicha waambie your past is place of reference not place of residence.
Sasa nalotaka kukuasa nimefuatilia interview zako kama mbili u tube nimeona swali kubwa waandishi wanalokimbilia kukuliza ni kama mali unazomiliki nyumba na magari Mumeo Uchebe ana mchango.
Na wewe ama kwa mahaba au kutunza heshima ya mume kama ilivyo ada kwa siye kina dada umekuwa ukijibu kwa bashasha "ana mchango mkubwa sana mtu sio lazima akupe pesa"
Mdogo wangu nakushauri acha kabisa hilo jibu hata kama ana mchango wa kimawazo hayo ni yenu ndani kwanza kuna mawili either wandishi wanauliza ivyo kummock mumeo wakijua hana mchango au yeye ndo anawatuma kupima upepo kwa sababu fulani anazozijua.Duniani usiamini mtu katika maisha hata mama yako .
Ingekuwa mimi ningewajibu ivi "mwanamke kuwa na mali haizuii kupendwa au kuolewa na mume asiye na kitu wengi tu wameoana hivyo wakaanza kutafuta pamoja mali ya mwenza aliyokuta inabaki yake ivyo basi nyumba na magari ni yangu binafsi ila Mungu atajalia tutatafuta zetu".Hapo hutaharibu heshima ya mumeo na akikasirika jua ana jambo,@miundombinu.Acha kabisa iyo kauli ya ana mchango mkubwa tu sio lazima pesa.Halafu mwanzoni hukuwa unajibu ivyo sijui nani kakuamsha.Nakupenda mpiganaji usijekulia kilio cha mbwa mwizi.Hawa miundo mbinu ni shida