Shilole: Nimekoma na ningejua hata nisingejichubua

Shilole: Nimekoma na ningejua hata nisingejichubua

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara ambaye pia ni msanii wa filamu, Zuwena Mohamed ‘Shilole' amefunguka kuwa kwa alichokiona, amekoma kutumia mkorogo.

Akipiga stori na Ijumaa, Shilole alisema mwanzo alikuwa akitumia mkorogo aina ya ‘karolaiti' lakini amegundua badala ya kumfanya awe mzuri zaidi, umemletea matatizo kwenye mwili wake.



Muigizaji ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki, Zuena Mohammed ‘Shilole'

"Niseme tu kwamba nimekoma na ningejua nisingefanya jaribio la kujichubua, nimeathrika sana na sijaona faida yoyote, zaidi umeniharibia ngozi yangu," alisema Shilole na kuongeza.


"Imefika wakati natamani niirudishe ile ngozi yangu ya asili lakini siwezi, sasa hivi nikiumia kidonda kinachukua muda mrefu kupona sababu ya huu mkorogo, warembo wanaojipenda ni bora wakaachana na mambo hayo.
 
KAROLAITI NDO INA MADHARA LAKINI DODO HAINA MADHARA KIAFYA.
Namshauri Shilole aanze kutumia Dodo.
 
KAROLAITI NDO INA MADHARA LAKINI DODO HAINA MADHARA KIAFYA.
Namshauri Shilole aanze kutumia Dodo.

Amesema mwanzo alikuwa anatumia "karolait" ujue mpk kufka kusema kashapaka vyote kamaliza, hawa wadada wa mjin (kama wanavyojiita) wana daktar wao huyo yupo kkoo ndio anayewauzia mabom hayo ya kujipaka..
ila mikorogo ina mwisho maana wote ni malalamiko, alianza dada kubwa wakafata wengine ss tupo kwa mziwanda's wife...
 
Kwenye kuchanganya L na R hua anaiacha hoiii huyuu
 
Ujinga tu na kutojiamini. Ni vizuri lakini coz mchuma janga hula na wakwao
 
Dinazarde hivi dodo haina madhara km carolaiti? Naomb unisaidie utaalam kdg nataka nijaribu
 
Back
Top Bottom