Shilole bado ana nia ya kugombea ubunge
kwenye jimbo lake la Igunga, lakini anahofia kuwa
maisha yake yanaweza kuwa hatarini!
Shilole ameiambia Bongo5 kuwa amepokea simu
nyingi kutoka Igunga zinazomtaka ajitose
kuwania nafasi hiyo, lakini bado yupo njia panda.
Unajua siasa ni ngumu mimi bado nipo kwenye
mjadala wa kugombea na hii ni baada ya kuona
watu wanataka kuongozwa, lakini bado nafikiria,
amesema. Nikiwa tayari nitagombea kupitia
CCM. Kitu ambacho kinaniogopesha kiukweli
ukiangaliwa watu waliopita ni vijana tu wanakufa
mapema kutokana na mambo ya siasa. Siasa
inahitaji moyo sana mimi ni muoga sana,
naogopa kufa watu wanauwana! Mtu unatamani
lakini ndo hivyo, ameongeza.
Mimi napigiwa simu nyumbani Igunga, watu
wengi sana kila mmoja ananiambia tunakuhitaji
ugombe yaani baada ya Rostam wananihitaji
mimi! Mimi bado nipo njia panda mpaka sasa hivi
lakini muda ukifika kila kitu mtasikia.
Chanzo bongo5