Shilole: Nitagombea Ubunge Igunga

Shilole: Nitagombea Ubunge Igunga

Shilole bado ana nia ya kugombea ubunge
kwenye jimbo lake la Igunga, lakini anahofia kuwa
maisha yake yanaweza kuwa hatarini!
Shilole ameiambia Bongo5 kuwa amepokea simu
nyingi kutoka Igunga zinazomtaka ajitose
kuwania nafasi hiyo, lakini bado yupo njia panda.
“Unajua siasa ni ngumu mimi bado nipo kwenye
mjadala wa kugombea na hii ni baada ya kuona
watu wanataka kuongozwa, lakini bado nafikiria,”
amesema. “Nikiwa tayari nitagombea kupitia
CCM. Kitu ambacho kinaniogopesha kiukweli
ukiangaliwa watu waliopita ni vijana tu wanakufa
mapema kutokana na mambo ya siasa. Siasa
inahitaji moyo sana mimi ni muoga sana,
naogopa kufa watu wanauwana! Mtu unatamani
lakini ndo hivyo,” ameongeza.
“Mimi napigiwa simu nyumbani Igunga, watu
wengi sana kila mmoja ananiambia ‘tunakuhitaji
ugombe yaani baada ya Rostam wananihitaji
mimi! Mimi bado nipo njia panda mpaka sasa hivi
lakini muda ukifika kila kitu mtasikia.”

Chanzo bongo5

Naogopa kuchoka kabla cjafanya kaxi Shilole???????Ubunge??????
 
"Kwa kuwa waliweza kulisukuma Basi mpaka upande wa pili, basi wakadhani na udereva wanaweza"
E. Mbogo-Moran.
Always simplicity is an enermy of truth.
 
Hivi ni wabunge gani waliofanya ubunge uonekane ni kitu rahisi sana?
 
juma nature. joseph haule. afande sele now shilole wa nuh ubunge huu
 
Hii habari mngechanganya na ile aliyosema anasubiri kolabo na JLO.
 
habari nyingine n za facebook na insta... sio uku jaman
 
Kwa design ya wabunge kama sugu na lema tena shilole anaweza kugombea uspika kabisa.
 
Yaani Sasa hivi wasanii wote wanataka kugombea ubunge...duh nchi hii jamani
Wabadilishe vigezo waweke vya elimu na degree watakimbia wote !
 
Hili nilikua napanda nyimbo zake now sipendi tena na asijidanganye atavuna aibu igunga imeiva kwa CHADEMA
 
Back
Top Bottom