Shilole: Nitagombea ubunge uchaguzi wa mwaka huu

Siyo zena ni zuwena mohamed na hana ufanya biashara wowote au mama ntilie ni biashara kubwa siku hizi tz
Mwanamziki nguli wa kimataifa na maarufu na mfanyabiashara mkubwa Tanzania Zena Yusuph Mohamed a.k.a shilole ametangaza nia yake ya kugombea Jimbo la Igunga ambapo pia ni sehemu alipokulia kwenye uchaguzi Huu wa mwaka 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwaka huu kuna werevu wengi watapigwa chini huku wapuuzi wengi wakiingia mjengoni
 
Akipewa ridhaa na atashinda. Kafumu ajiandae kura za maoni. Hata Sugu alivyogombea mara ya kwanza hakuna aliemdhania atashinda.
Huwezi kumlinganisha Sugu na vimbwenelehi hata kidogo. Sugu amekuwa mwanaharakati katika maisha yake yote na muziki wake ni wakiharakati sio hivyo miziki ya inama inuka.
Uanaharakati pekee waweza kuwa sifa ya kuwawakilisha watu kuwatetea. Shilole anajua nini anachoweza kukipigania? CCM wameudharaulisha ubunge na kuwa kazi takataka
 
Hakika naitazama ccm ikipoteza mvuto hata kwa sisi makada wake muhimu.

Shilole anatarajiwa kugombea ubunge hapa kwetu igunga na kwa hali ilivyo ndani ya chama chetu atapitishwa tu.

Harmonize atapitishwa kule Tandahimba hiyo haina ubishi, maana mwenye chama kasema.

Mimi na makada wenzangu wenye msimamo wa kati ndani ya ccm tumeanza kujiweka kando ili kuwapisha wabunge hawa wasanii ili wakafanye usanii pale bungeni dodoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…