Tangu 2015 watanzania hatujapata rais anayestahili na mwenye sifa za uongozi.
Rais wa 2015 - 2021 .
Huyu alikuwa anaendesha nchi kama nyumba yake. Alijawa na sifa za kishamba, matusi kibao na udikteta usioelezeka. Alitaka kila kitu kiwe siri, kuanzia mikopo inayochukuliwa na serikali mpaka magonjwa kama kipindupimdu, Zika na korona.
Aliharibu mizizi na mishipa ya kiuchumi kwa kuwachukia, kuwapora na kuwafilisi wafanyabiashara. Aliendesha nchi kwa kukandamiza kila kundi nchi hii. Uchumi aliudidimiza.
Serikalini alijaza ndugu na kabila lake ambalo ndiyo walikuwa wakiiba na kutafuna fedha ya nchi hii.
Aliichukia demokrasia kabisa, aliiba uchaguzi na alizima internet siku ya uchaguzi, na baadaye kuwafanya baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuhama nchi. Na mbaya zaidi alitungas heria kandamzi za habari na wanahabari na alianzisha kikundi cha wasiojulikana.
Wa 2021 - mpk sasa.
Rais wa sasa kinchomharibia ni ulaghai. Anatoa ahadi nyingi zenye muelekeo mwema lakini kumbe deep down her soul hakusudii kutimiza ahadi yake. Aliwafurahisha wapinzani kwa mazungumzo marefu ya maridhiano ambayo mwisho wa siku yalikuwa danganya toto. Akaanzisha kikosi kazi cha kuunda tume huru , lkn kumbe hakumaanisha, aliahidi katiba mpya nayo pia amechomoa.
Pia rais huyu, inaelekea serikali yake "imepigwa kopi na wahuni" (msemo wa H. Polepole), ama kwa maneno ya mwalimu Nyerere tunasema serikali ya mama "imewekwa mfukoni". Anaonekana kapokwa madaraka kabisa, kubakia na cheo cha urais tu, lkn serikali inaendeshwa na wahuni.
Fedha za serikali zinachotwa mama hasemi, bei za bidhaa zinapanda hovyo mama hasemi.
2025 tunawataka watanzania wote wenye akili, wenye nafasi ndani ya jamii, ndani na nje ya ccm/serikalini, mfanye jambo litakaloinusuru nchi hii. Tunahitaji mtu atakayekuwa na sifa za uongozi, siyo uongozi wa sifa.