KERO Shimo Kubwa katikati ya barabara Shekilango Latishia Usalama wa Watumiaji wa Barabara, Mamlaka Husika Hawaoni Hili?

KERO Shimo Kubwa katikati ya barabara Shekilango Latishia Usalama wa Watumiaji wa Barabara, Mamlaka Husika Hawaoni Hili?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mkweliwatz

Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
8
Reaction score
11
20260626_205108.jpg
Shimo kubwa lililopo katikati ya barabara eneo la Shekilango mara tu baada ya tuta, limeendelea kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara. Kutokana na ukubwa wake madereva hulazimika kulikwepa ghafla jambo linaloongeza hatari ya ajali na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo

Licha ya barabara hiyo kutumiwa na idadi kubwa ya magari kila siku, shimo hilo bado halijafanyiwa matengenezo hali inayozua maswali kuhusu kasi ya mamlaka husika kushughulikia changamoto zinazohatarisha usalama wa wananchi.

Je, mamlaka husika hazijaliona shimo hili, au zinasubiri litokee tukio la kusikitisha ndipo zichukue hatua
 
Hayo mashimo yamejaa karibu barabara zote za Dar tena shukuru hapo mvua haijanyesha kuna hii njia ya km unatoka Majumba 6 Stakishari unaelekea Daraja la Kinyerezi njia ya Segerea kuna Shimo moja hatari sana nilikuta jamaa ameacha matairi yote ya mbele aliparamia shimo kudadek shimo likapita na matairi ya mbele
 
View attachment 3619417Shimo kubwa lililopo katikati ya barabara eneo la Shekilango mara tu baada ya tuta, limeendelea kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara. Kutokana na ukubwa wake madereva hulazimika kulikwepa ghafla jambo linaloongeza hatari ya ajali na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo

Licha ya barabara hiyo kutumiwa na idadi kubwa ya magari kila siku, shimo hilo bado halijafanyiwa matengenezo hali inayozua maswali kuhusu kasi ya mamlaka husika kushughulikia changamoto zinazohatarisha usalama wa wananchi.

Je, mamlaka husika hazijaliona shimo hili, au zinasubiri litokee tukio la kusikitisha ndipo zichukue hatua
Gentleman,
ni muhimu sana kuripoti kwenye mamlaka husika bila kusubiri na wao waone kama ulivyoona wewe, na itapendeza zaidi 🐒
 
Waziri wa ujenzi ni mtaalamu wa uvuvi akitokea Mkuranga mahali ambapo wengi hawajaona lami.
 
Kuendesha barabara hujawahi ipita bongo umakini uwe 100%!!

Mkoa hapo boda wangeshatundika reflector kuokoa jahazi.
 
Back
Top Bottom