View attachment 3619417Shimo kubwa lililopo katikati ya barabara eneo la Shekilango mara tu baada ya tuta, limeendelea kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara. Kutokana na ukubwa wake madereva hulazimika kulikwepa ghafla jambo linaloongeza hatari ya ajali na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo
Licha ya barabara hiyo kutumiwa na idadi kubwa ya magari kila siku, shimo hilo bado halijafanyiwa matengenezo hali inayozua maswali kuhusu kasi ya mamlaka husika kushughulikia changamoto zinazohatarisha usalama wa wananchi.
Je, mamlaka husika hazijaliona shimo hili, au zinasubiri litokee tukio la kusikitisha ndipo zichukue hatua