Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change 2022)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change 2022)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
SOC 2022 (1).png

SOC 2022 (2).png
Jamii Forums, Asasi ya Kiraia inayohamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora na mratibu wa jukwaa la mtandaoni la JamiiForums.com (JF), imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (Citizen Journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi na wananchi wenzao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai.

Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye awamu nyingine ya shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko chanya (Stories of Change).

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Awamu hii ya pili ya shindano hili itafanyika Julai 15 hadi Septemba 15, 2022.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  1. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
  2. Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
  3. Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
  4. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
  5. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  6. Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.

Jinsi ya kushiriki:
Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili.

Maandiko yawasilishwe kuanzia Julai 15 hadi Septemba 15, 2022 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )

Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.

ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Vigezo vya kupata Washindi
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura/likes zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.

Ni muhimu kuendelea kuwa ‘active’ katika jukwaa la JF muda wote wa shindano ili kurahisisha mawasiliano endapo utaibuka mshindi.

Zawadi kwa Washindi
Mshindi wa Kwanza Tsh. 5,000,000
Mshindi wa Pili Tsh. 3,000,000
Mshindi wa Tatu Tsh. 2,000,000
Mshindi wa Nne Tsh. 1,000,000
Mshindi wa Tano Tsh. 500,000
Mshindi wa Sita hadi kumi Tsh. 300,000
Mshindi wa Kumi na Moja hadi wa Ishirini Tsh. 200,000

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 116
Jamani kua
KWA HIYO ILI KUINUSULU JAMII KUTOKANA NA JANGA LA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA PAMOJA NA BIMA YETU TAIFA(NHIF)JAMII IFANYE YAFUATAYO.
Kwa hiyo ili kuinusuru jamii kutokana na janga la magonjwa yasiyo ambukiza nchini na ulimwengu kwa ujumla hapo hapo tutakuwa pia tumeinusuru bima yetu ya taifa(NHIF) tukubali kubadilika kwa kufanya yafuatayo:
Tupunguze ama tuache kula vyakula ambavyo havina faida katika mihili yetu ambavyo Mara nyingi utusababidhia maradhi tu
Ksma tulivyo eleza hapo nyuma miongoni mwa vyakula hivyo na vinywaji ni kama
Epuka kula Vyakula vyenye mafuta mengi
Epuka kula vyakula vya kukaanga Mara kwa Mara au mda wooote
Punguza matumizi ya chumvi nyingi katika mboga au kunyunyuzia pembeni kama katika mahindi badala take tumia viungo kama vile ndimu, limau ,pilipili. Kwa sababu chumvi inasababisha sanaaa (BP) ambalo linaongoza kusababisha figo kufeli(Renal failure)
Punguza matumizi ya vinywaji vyenye sukari Mara kwa Mara kama vile sodas, juisi za viwandani ili kuepuka kupata kisukari (Diabetes) ambacho kinaongoza kusababisha figo kufeli(Renal failure)
Watu tupunguze kula vitu vilivyo kaangwa (trans-fats) au vilivyo rostishwa Mara kwa Mara ili kupunguza hatari ya mafuta kuganda katika mishipa ya damu na kusababisha (atherosclerosis) na kusababisha maradhi ya moyo, pressure (BP) na kiharusi (Stroke)
Watu tufuatilie hali ya uzito wetu Mara kwa Mara kwani kuwa na uzito mkubwa ni chanzo kikubwa cha maradhi ya
MOYO
KIHARUSI
PRESSURE(BP)
DIABETES (KISUKARI)
KUFELI KWA FIGO
Ufanyaji wa mazoezi watu tufanye sanaa mazoezi tunatakiwa tufanye mazoezi angalau nusu saa(30) kwa siku na kwa wiki Massa mawili na nusu hapo utakuwa fiti kabisaa na haya magonjwa yasiyo ambukiza utayasikia tuu katika bombs na kupelekea kuishi miaka mingiii.
Ndugu zanguni magonjwa yasiyo ambukiza yanakatisha uhai mapema sanaaa ama husababisha vifo vya mapema Ulimwengu nzima kwa hiyo kula vizuri fany mazoezi uishi sanaaa
Kwa kufuata haya tunaweza kuinusuru bima yetu ya taifa(NHIF) na sisi wenyewe kusalimika na janga hili linalo tumaliza kwa sasa la magonjwa yasiyo ambukiza ambalo yamekuwa kwa sasa ndio yanaua watu wengi balaaa duniani kwa sasa ndio kimekuwa kilio kula pembe ya dunia uzuri wake yamekuwa hayachagui masikini wala tajiri, kiongozi mkubwa au raia wa kawaida yao yanaua tuu.

Kwahiyo wito wangu kwenu tubadilike haya maradhi yanatumaliza.
Jamani kuandika kote Kyle si kubahatika kuchaguliwaaa.
 
Naombeni kura zenu hata kama sijashindana naitaji kuangalia je nimeendelea Uandishi wangu nishapishe kitabu , Tufanye nini tuboreshe elimu yetu na Linda afya jina Kisesa2022

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom