Jamii Forums, Asasi ya Kiraia inayohamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora na mratibu wa jukwaa la mtandaoni la JamiiForums.com (JF), imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (Citizen Journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi na wananchi wenzao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai.
Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.
Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye awamu nyingine ya shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko chanya (Stories of Change).
Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.
Awamu hii ya pili ya shindano hili itafanyika
Julai 15 hadi Septemba 14, 2022.
Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:
- Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
- Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
- Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
- Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
- Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
- Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.
Jinsi ya kushiriki:
Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu
kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (
www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili.
Maandiko yawasilishwe kuanzia
Julai 15 hadi
Septemba 14, 2022 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (
Stories of Change )
Baada ya kuweka andiko lako jukwaani,
JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.
Vigezo vya kupata Washindi
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura/likes zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%).
Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.
Ni muhimu kuendelea kuwa ‘active’ katika jukwaa la JF muda wote wa shindano ili kurahisisha mawasiliano endapo utaibuka mshindi.
Zawadi kwa Washindi
Mshindi wa Kwanza Tsh. 5,000,000
Mshindi wa Pili Tsh. 3,000,000
Mshindi wa Tatu Tsh. 2,000,000
Mshindi wa Nne Tsh. 1,000,000
Mshindi wa Tano Tsh. 500,000
Mshindi wa Sita hadi kumi Tsh. 300,000
Mshindi wa Kumi na Moja hadi wa Ishirini Tsh. 200,000
Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe:
stories@jamiiforums.com
UNAYEHISI UMECHELEWA KUFANIKIWA, HII NDIO NJIA YA MKATO
Makala hii inahusu mafanikio maishani kwenye pembe ya kiuchumi au katika swala la kifedha. Katika kutambua umechelewa au laa!. Mara nyingi jukwaa la umri ndio hutaja muda uliogawanywa katika nyakati tofauti ziendanazo na majukumu fulani.
Nyakati katika maisha zimewekwa ndani ya kifurushi cha muda, dhana ya kuwahi au kuchelewa hua na tafsiri tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine kwakua kuna vitu hututofautisha kama;
- Vipaombele vya maisha
- Aina ya maisha
- Viwango vya maisha
Kuna anaye amini kuna kuchelewa na kuna asiye amini. Japo mafanikio huweza kuja muda wowote ambao juhudi na mikakati sahihi vitaenda sambamba. Neno kuchelewa haliepukiki kwakua muda na mgawanyiko wa majukumu kwa mwanadamu vitakuwepo tu.
Colonal Sanders mwanzilishi wa KFC alianzisha mgahawa huo akiwa na miaka 65. Juhudi na kutokukata tamaa bado vina nafasi katika kutimiza maono.
Vitu, wanyama, hali na watu vimejikita katika muda. kila jambo na wakati wake. Hivyo muda unaweza kutueleza tumekwenda sambamba nao, tumeuokoa au tumechelewa;Mfano;
-Pumzika kwa amani
-Tarehe ya kuzaliwa na tarehe ya kufa. Viumbe hai huishi katika muda na kuna muda havitoweza kuishi na kufanya majukumu
-Tarehe ya kikomo cha matumizi
-Tarehe ya kutengenezwa na tarehe ya mwisho wa matumizi. Iwe katika bidhaa za kula au hata vitu vingine
-Kustaafu
Kuajiriwa na kikomo cha ajira. Umri utasema nenda kapumzike katika majukumu haya
NINI SABABU ZA KUCHELEWA KUFIKA KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO?
Hizi ni baadhi ya sababu;
1. Mtu mwenyewe
Mtu mwenyewe anaweza kujichelewesha kutokana na tabia kama matumizi mabaya ya muda, kukosa maono, kutapanya fedha na kukosa vipaombele .
2. Kucheleweshwa na ndugu,jamaa au marafiki
Pale ambapo mtu anaweza kukosa kiasi katika kutoa msaada wa kifedha au anaishi maono yao kwa kufungamana nao kupitia maamuzi ya pamoja pasipo kuangalia yanashahabiana na ndoto zake au laa!.
3. Kucheleshawa na hali
Mfano vita, magonjwa na majanga
4. Mila na desturi
Kuna mila na desturi zinazoweza kumchelewesha mtu kufanikiwa au asiweze kufanikiwa kabisa. Mfano mila ambayo inakataza mwanamke kufanya shughuli za uzalishaji na kua tegemezi kwa mume, muda mume kafariki au wametengana itamfanya kuanza mwanzo akiwa haelewi aanzie wapi kuweza kuhudumia familia pia kufika kilele cha mafanikio atamaniyo.
EPUKA MAMBO YAFUATAYO UHISIPO UMECHELEWA
1. Kutoishi ndoto zako
Ndoto kama maono ni picha uitengenezayo akilini ikufanyayo kua na bidii ili iweze kutokea katika uhalisia .Hata kama unahisi umechelewa ni vema kuishi ndani ya ndoto. Mara nyigi ndoto huleta msukumo na kuongeza hari , hamasa pia kumfanya muotaji asikate tamaa.
2. Kujihisi mwenye mkosi
Bidii ni baba wa bahati njema, Bahati hutokana na bidii sio kinyume
3. Kutaka matokeo hafifu
Vema kubaki katika viwango vile ulivyovitamani ili hari na bidiii iwe kubwa. Vema kupambana kwa nguvu sababu unaweza kutamani vidogo na kujikuta huvipati kwa kufanya mambo kwa ulegevu kupelekea kutoona matokeo katika dunia ya ushindani
4. Kukosa mpango wa pili
Vema kua na mpango mbadala, pale ambapo wa awali hauleti matokeo unafanya wa pili. Itasaidia hatma kutopotea moja kwa moja pia huweka vema saikolojia pale mpango wa awali unapofe, swala la biashara, utoaji wa huduma ama kipaji huzingatia saikolojia sababu kuna vitu kama hofu, woga pia maamuzi
5. Kutafuta njia za mkato au mafanikio ya haraka
Njia za mkato ni hatari iwe kukwepa kodi, ujambazi na utapeli. Ni vitu ambavyo huzima ndoto na hupelekea kufilisiwa, kifungo pamoja na vifo. Jambo la msingi ni kuhakikisha mchakato wote ni halali kwa sheria, kanuni na taratibu za nchi
6. Kulalamika na kulaumu
Haijawahi kuleta suluhisho. Acha kulaumu mifumo, serikali na watu. Hukuongezea tuu chuki,visasi na maumivu. Ambavyo ni hatari kwa afya ya mwili na akili. Kikubwa ni kutumia vema muda.
Kazi za muda ni
- Kutafuta mawazo mapya
- Kufikiri
- Kuandaa mazingira
Muda usipotumika vema lazima changamoto za umasikini zijitokeze kwa sababu muda ni rasilimani ambayo hufanya msaada katika uzalishaji ndio sababu watu hununua muda wa watu wengine kwa kuwaajiri na wao waajiri hujiongezea muda wa kufanya kazi kupitia watu.
Kutomtegemea Mungu
Soma vitabu vya kiimani. Hutuelekeza katika majukumu ,subira na uwajibikaji, Hutujengea imani ambayo hutupa mwanga kwa kila hatua. Vema kuhudhuria nyumba za ibada na kutoa sadaka ili kufungua milango ya mafanikio na kujiungamanisha na Mungu aweze kusimama katika changamoto.
NINI KIFANYIKE PALE UHISIPO KUCHELEWA?
Hatua 6 zinaweza kukuongezea kasi na kufanikiwa kupitia njia chanya
1.AWALI
2.HABARI
3.HATARI
4.AMALI
5.KIBALI
6.MALI
AWALI
Ni mwanzo. unaanza na wazo la biashara kwa kuliweka kwenye makaratasi. Wazo liwe linaloweza kutatua changamoto za watu. linaloweza kuja kutokana na kipaji, ujuzi,taaluma hata uzoefu.
HABARI
Kutafuta taarifa kuhusu wazo kwa kufanya tafiti . Soma vitabu vihusianavyo na wazo lako , fwatilia wakufunzi kwenye mitandao ya kijamii na kufanya mambo mengi ya muhimu yatakayo kusaidia kutofeli kizembe
HATARI
Kama unaogopa kukosea huwezi kufanya. Chochote ufanyacho kitaleta majibu iwe ni hasi au chanya, Ni vema kuiambia akili hivyo ili hata mambo yakienda kinyume na matarajio ujipange tena
AMALI
Amali ni vitendo, unaanza baada ya kujiridhisha na taarifa ulizopata pia na maandalizi mengine kama kukamilisha taratibu zote za kisheria.Usianze pale walipo wenzio bali anza hatua moja mbele zaidi, simaanishi kwa swala la ukubwa bali ubunifu.
KIBALI
Ukifanya vema , utaanza kutengeneza jina na kuanza kuzoeleka na wateja, ni hatua nzuri. Epuka kutojali wateja, kuridhika pia uvivu. Hakikisha ubora ni wimbo wako hata ukipata wasaidizi waimbishe sio kuona wateja watanunua tuu. Wapinzani hawalali, kama huwaoni amini siku moja watakuja.
MALI
Ni hatua kubwa ya mafanikio, fedha inapoanza kuonekana ikiwa ni faida itakayo pelekea kufungua matawi,mtaji kukua na kuaminika zaidi, iwe ni ndani ya mtaa, mkoa, nchi hata ngazi za kimataifa.
HITIMISHO
Jaribu kua mtulivu kifikra na kutopoteza hari. Amini hali inaweza kubadilika. Vema uchukulie kuchelewa ni nafasi ya kujifunza kutokana na makosa, fursa ya kukufanya ufanye vema, sababu ya kufanikiwa zaidi pia ni fursa ya kulinda ulichonacho sababu muda umekwenda.
“
Kuna makundi matatu ya watu,kundi la kwanza ni wale wanaotaka jambo litokee. Kundi la pili ni wale wanaotamani jambo litokee na kundi la tatu ni wale wanaofanya jambo litokee” alisema Michael Jordan