View attachment 2291152
View attachment 2291153
Jamii Forums, Asasi ya Kiraia inayohamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora na mratibu wa jukwaa la mtandaoni la JamiiForums.com (JF), imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (Citizen Journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi na wananchi wenzao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai.
Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.
Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye awamu nyingine ya shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko chanya (Stories of Change).
Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.
Awamu hii ya pili ya shindano hili itafanyika
Julai 15 hadi Septemba 14, 2022.
Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:
- Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
- Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
- Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
- Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
- Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
- Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.
Jinsi ya kushiriki:
Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu
kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (
www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili.
Maandiko yawasilishwe kuanzia
Julai 15 hadi
Septemba 14, 2022 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (
Stories of Change )
Baada ya kuweka andiko lako jukwaani,
JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.
Vigezo vya kupata Washindi
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura/likes zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%).
Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.
Ni muhimu kuendelea kuwa ‘active’ katika jukwaa la JF muda wote wa shindano ili kurahisisha mawasiliano endapo utaibuka mshindi.
Zawadi kwa Washindi
Mshindi wa Kwanza Tsh. 5,000,000
Mshindi wa Pili Tsh. 3,000,000
Mshindi wa Tatu Tsh. 2,000,000
Mshindi wa Nne Tsh. 1,000,000
Mshindi wa Tano Tsh. 500,000
Mshindi wa Sita hadi kumi Tsh. 300,000
Mshindi wa Kumi na Moja hadi wa Ishirini Tsh. 200,000
Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe:
stories@jamiiforums.com
NITAWEZA...
Nilianza kujitambua nikiwa kituo cha watoto yatima, kujijua kuwa mimi ni nani..
Yakuwa mimi sina wazazi! Mimi ni yatima...
Niliwahi kumuuliza mlezi wetu
'Madam mimi nilifikaje hapa?'
Awali hakupenda kunielezea nafikiri alijua muda bado...lakini baadae nilipomuuliza tena na tena ndio akaweza kunielezea....akiongea kwanza kwa kunishauri, kuwa nisijali, kwasababu, huwezi kujua ni kitu gani kilimfanya mama yangu afanye hivyo...
‘Kwahiyo mimi nililetwaje hapa kituoni na nani..?’
‘Uliokotwa jalalani...’akasema
‘Nini.....?’
Kiukweli, nilishtuka sana,..ilikuwa kama mtu kanipiga na kitu kichwani na kupotea fahamu kwa sekunde kadhaa...nilihisi vibaya..Hata hivyo nilitamani nimuone mama yangu japo niijue sura yake!..!
Ndio, kuna kipindi nawaza na kuwazua ilikuwaje mama ahangaike miei tisa, halafu keshanizaa, aende kunitupa jalalani, nilikuwa kama siamini vile..
‘Lazima kuna sababu ya mama kufanya hivyo....huenda hata sio kosa lake...’nilisema hivyo, nilipoweza kuongea na mlezi wangu..na ni kweli moyoni nilimsamehe...!
Siku zikaenda , shule sikuwa vizuri.. labda kutokana na kuwaza sana, nilikuwa nawaza sana, hata kulia,...na kwa kujitetea, kutokufanya vizuri huko, labda kulitokana nahali zetu kituoni hapo, maana tulikuwa tunaishi kwa kutegemea misaada, kuna kipindi tunakosa...tunageuka kuwa omba omba!.
Mlei wezi, hakukata tamaa, na nilimuona ndiye mzazi wangu, hata nikikosa amani, huwa ninamuendea, nakaa karibu naye, nalala mapajani kwake,...alitupenda kama Watoto wake, yeye hakubahatika kupata mtoto...na alikuwa akisema
‘Mungu hakunijalia kizazi, na ninajua ni kwanini....ni ili nije kuwalea nyie...’akasema
Kuna maneno yake ambayo yalinipa hamasa sana kwenye maisha yangu ya kila siku....`kuwa tutawea....alikuwa akituambai hivi;
'Watoto wangu katika maisha haya kamwe msikate tamaa , haya yote ni maisha tu... , wapo Watoto wenye wazazi na kila kitu lakini bado hawana raha, bado hawafanikiwi katika maisha yao, na wengine wazazi wao ni Zaidi ya nyie, wazazi hawana kitu, wanaishi maisha ya dhiki kabisa..
'Kwahiyo jipeni moyo..maana yote haya ni maisha tu...uwe na mzazi au usiwe na mzazi kila mtu ana njia yake ya mafanikio.. ilimradi tu, uwe na afya njema, uwe na bidii na uwe na malengo yako ya kimaisha, na Zaidi muishi kwenye maadili mema kama nilivyowalea, mkifanya hivyo; MTAYAWEZA MAISHA...'
'Nitaweza..' ikawa sasa ndio kipaumbele change, cha kunipa moyo.Kila jambo nikishindwa najipa moyo kuwa nitaweza tu...najibidisha kuliweza...na mara nyingi nafanikiwa, nispofanikiwa bado ninasema ipo siku nitaweza...!
********
Umri ukawa unakwenda shule kidato cha nne niliponea chupuchupu kupata zero...!
Nilijua sasa natakiwa nifanye jambo sitaweza kuishi na mlezi wetu milele, nifanyaje sasa...natakiwa niweze kuishi, niwe na mimi na kwangu, niweze kujitegemea..ila sikupenda kuolewa, moyo wangu ulinituma kuwa natakiwa nisimame mimi kama mimi...!
Wakati itukiwa kituoni, kulikuwa na vipindi vya michezo, mimi nilipendelea sana kuigiza. Na kwenye kikundi chetu cha maigizo, nilitokea kufanya vizuri, hadi kuitwa muigizaji bora..
‘Nitakuwa muigizaji mkuu, kama....’niliwaza hivyo.., nikiwakumbuka waigizaji wakuu niliwahi kuwaona kwenye runinga!
Hapo sasa ikawa kazi ya kuwatafuta watu wanaofanya hiyo kazi....niliwauliza watu wanaowafahamu na bahati nikaweza kuwapata baadhi yao.
Sikutarajia kuwa kutokana na historia ya maisha yangu, yangenikuta yaliyonikuta, kwa maana kila niliyekutana naye, nilijaribu kumuelezea maisha yangu!..Ni kweli nijaliwa umbo zuri, sura nzuri, lakini kamwe sikupenda na sitapenda....kuzalilishwa...moyoni niliapa hilo!
Wa kwanza kukutana naye, baada ya kunisikilia, akasema;
‘Twende ofisini kwangu...’
Nikajua ehee..bahati ndio hiyo. Nikafika ofisini kwake, mara mlango ukafungwa, akaniangalia kwa muda, halafu akasema;
‘Wewe unajiamimi kweli kwa maana kazi hizi wanatakiwa watu wanaojiamini...’
‘Ndio najiamini...’nikasema kwa kujiamini.
'Vua hayo mavazi yako ya kujifunika funika,...nataka nikuone vyema, ulivyoumbika...wewe ni mrembo!...’akasema
Hapo moyo wangu ulishituka, sikupenda, na mlezi wetu alituoanya sana kuonyesha maumbile yetu wanaume, lakini nikajua labda ndivyo itakiwavyo!
Nikafanya kama alivyonielekeza...mara, nashikwashikwa..alipojaribu zaidi...nilijikuta tu mguu goti limefanya kazi yake...sikumchelewesha nilishahisi lengo lake! Kuna namna tulifundishwa kituoni jinsi ya kujihami kama ikitokea mwanaume anataka kukuzalilisha, kwenye mazoei ya kujihami Nashukuru sana mazoezi ya kituoni yalinisaidia sana..!
Sikukata tamaa nikijua huyo labda ni tamaa zake ngoja nikajaribu sehemu nyingine..
Wa pili niliyekwenda kwake,...ilitokea hivyo hivyo, ila siku hiyo kuna mafuta nilikwenda nayo ya kupuliza, hiyo ni silaha nyingine tulifundishwa, na huyo jamaa alipotaka kuleta za kuleta,...nilimpulizia mafuta hayo machoni,....huyu kiukweli alitaka kunibaka....nikakimbia.
Nikajua sasa... kumbe huko hakunifai...huenda huko sio njia yangu!
Umri unasonga mbele...natakiwa niishi, nile nivae.. na umbile langu limeshaanza kuwa mtihani, kila mwanaume ananitamani....nilipitia changamoto hizo hasa nikiwa na shida!
Mimi moyoni nilisha-apa kamwe sitazalikika, kamwe sitapenda nizae nimtupe mtoto wangu, kama nilivyofanyiwa mimi...ahadi kwangu ni deni!
Nilifuata ushauri wa mlezi wangu...kuwa kamwe nisikubali mwanaume auguse mwili wangu, kamwe nisivae kizembe kwa kuacha sehemu ya mwili wangu wazi, niliozea hivyo!
Hata hivyo, kama msichana, nilipenda kuvaa vizuri, kupendeza lakini vyovyote nitakavyovaa mwili wangu niliusitiri..usingeliweza kuniona mitaani nimevaa kinyume na maadili...nilijua kwa jinsi nilivyofundishwa, kujilinda kwangu ni pamoja na kutokuwashawishi wanaume..
Baadae niliamua kuwa yaya..napenda sana watoto, nikapata kazi za ndani, mama mwenye nyumba ni mfanyakazi na baba pia. Wanaondoka asubuhi wanarudi usiku. Mimi nilikaa na Watoto, kuwapikia, kuwafulia, na kila kitu, nilipendezewa sana na maisha hayo!
Siku moja usiku nimelala .. nashtuka kitu kinanipapasa matiti..nataka kupiga kelele nikazibwa mdomo...sikukubali...mguu wangu ulitosha kujiokoa.
Nilitoka usiku huo huo na kutokomea mitaani..lakini baada ya kuhakikisha mbaba yule kabakia na maumivu. Nilimpiga kigoti, na nikikupiga kigoti, lazima utaumia tu!
Baada ya kuikosa hiyo kazi, nililia sana, kiukweli niliipenda, na wale Watoto niliwapenda, walishanizoea, nahisi watakuwa wananililia, lakini sikupenda kurudi tena hapo kazini.
Nililala nje usiku huo...ndio nikaota kuwa nitaweza lakini nisiishi kwa kuwategemea watu...nibuni kitu...ndoto ile haikuendelea,...iliishia hapo,’nibuni kitu’...
Nibuni nini !...sikujua, nikaamuka, nikaanza kumuomba mola wangu.
Kwenye maombi haya kwa mola, kiukweli nilitoa machozi....nikimlilia mola wangu anionyeshe sababu ya kulipata fungu langu la riziki kihalali...nisiendelee kuzalilika tena!
Nikakumbuka jambo....
Wakati tukiwa kituoni tulikuwa tunasukana.. nilikuwa napenda kuwasuka wenzangu..ile kupenda kuwasuka wenzangu kulinijengea ujuzi wa kusuka, vidole vyangu vilikuwa vyepesi kwenye ususi...nikahisi naweza kulijaribu hilo...
Nilianza tu kama mchezo, nikimuoma mwanamama, namuuliza...unataka kusuka, mimi najua kusuka nywele, akikubali ninamsuka...!.
Nilianza na mtu mmoja mmoja...nasuka kwa malipo kidogo!
Kipaji hicho kilinisaidia..na kila hatua nilijifunza zaidi, nikabuni mitindo zaidi!..kidogo nilichopata likanijia wazo la kujisomesha kuujua zaidi ususi . Nilifanya hivyo, na mola akanisaidia, nikawa MSUSI MNZURI!
Hutaamini...niliweza..na sasa nina saluni yangu binafsi!
NIlILOJIFUNZA...usikate tamaa kama bado una pumzi, na kwenye kuhangaika usitegemee mtu, mtegemee mola wako, muombe mola wako akuonyeshe kipaji chako, kwa maana kila mtu ana kipaji chake na mola pekee ndiye muongozaji...hutaamini...UTAWEZA TU!
Name; emuthree
Tel 0787366097