Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change 2022)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
SOC 2022 (1).png

SOC 2022 (2).png
Jamii Forums, Asasi ya Kiraia inayohamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora na mratibu wa jukwaa la mtandaoni la JamiiForums.com (JF), imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (Citizen Journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi na wananchi wenzao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai.

Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye awamu nyingine ya shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko chanya (Stories of Change).

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Awamu hii ya pili ya shindano hili itafanyika Julai 15 hadi Septemba 15, 2022.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  1. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
  2. Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
  3. Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
  4. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
  5. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  6. Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.

Jinsi ya kushiriki:
Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili.

Maandiko yawasilishwe kuanzia Julai 15 hadi Septemba 15, 2022 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )

Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.

ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Vigezo vya kupata Washindi
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura/likes zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.

Ni muhimu kuendelea kuwa ‘active’ katika jukwaa la JF muda wote wa shindano ili kurahisisha mawasiliano endapo utaibuka mshindi.

Zawadi kwa Washindi
Mshindi wa Kwanza Tsh. 5,000,000
Mshindi wa Pili Tsh. 3,000,000
Mshindi wa Tatu Tsh. 2,000,000
Mshindi wa Nne Tsh. 1,000,000
Mshindi wa Tano Tsh. 500,000
Mshindi wa Sita hadi kumi Tsh. 300,000
Mshindi wa Kumi na Moja hadi wa Ishirini Tsh. 200,000

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 116
View attachment 2291152
View attachment 2291153
Jamii Forums, Asasi ya Kiraia inayohamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora na mratibu wa jukwaa la mtandaoni la JamiiForums.com (JF), imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (Citizen Journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi na wananchi wenzao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai.

Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye awamu nyingine ya shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko chanya (Stories of Change).

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Awamu hii ya pili ya shindano hili itafanyika Julai 15 hadi Septemba 14, 2022.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  1. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
  2. Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
  3. Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
  4. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
  5. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  6. Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.

Jinsi ya kushiriki:

Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili.

Maandiko yawasilishwe kuanzia Julai 15 hadi Septemba 14, 2022 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )

Nitashiriki.......✍️
 
iandike kwenye jukwaa la stories of change Kama thread.
Mbona nimepost wanasema sijuh mpka ikaguliwe na amdeveloper ndio itaanz kuonekan kwa umma tangu saa 8 mchan mpaka saiz haijaanz kuonekan mimi siioni kam imepostiwa kwanin?
 
Yeah ipo hivyo hata baadhi ya post ukireply Ila SEMA hii baada ya kupost thread inatoa taarifa kuwa haionekani Kwa umma hawajasema kuwa utaiona wewe peke yako tofauti na utakaporeply thread yoyote, hivyo itakuwa moderators wanapitia maudhui
 
Nashukur ndugu yangu basi wacha niendelee kusubir asnte kwa majibu yako
 
Mmeondoa Syory zanhu mbili na zisha pata michango na kupigiwa juta, shirikini wenyewe ba watu mlio waandaa.

Hamuwrzi ondoa poat zina siku 3 then hamtoi sababu ya kuziondoa.
 
Yeah ipo hivyo hata baadhi ya post ukireply Ila SEMA hii baada ya kupost thread inatoa taarifa kuwa haionekani Kwa umma hawajasema kuwa utaiona wewe peke yako tofauti na utakaporeply thread yoyote, hivyo itakuwa moderators wanapitia maudhui
Mimi nashangaa post mbili wameziondoa hakuna sababu ya kuziondoa na zina siku kadha, zisha pigiwa hadi kura.
 
Mmeondoa Syory zanhu mbili na zisha pata michango na kupigiwa juta, shirikini wenyewe ba watu mlio waandaa.

Hamuwrzi ondoa poat zina siku 3 then hamtoi sababu ya kuziondoa.
zilikuwa na title ipi mkuu
 
MGANGA TOKA SUMBAWANGA

tunaroga na kuwapumbaza watakao pitia maandiko ya story of change ili wakuchague wewe kuwa mshindi

Malipo n kidogo Sana karibuni pm
 
Mimi nashangaa post mbili wameziondoa hakuna sababu ya kuziondoa na zina siku kadha, zisha pigiwa hadi kura.
Mimi sizani kuziondoa Ina maanisha vibaya kwani hata thread yangu niliyopost wameiondoa haikumaliza hata dk 1 Wacha tusubiri labda wabobezi wakipost zao zitaachwa🙌🙌
 
Mwenye shida na hela anione nimwandikie.
😂😂😂😂Kwa iyo wewe utaki ela, lakini pia wazo lako ukilitoa moja kwa moja litakua na mantiki zaidi na pia utakua na nafasi kubwa ya kulitetea na kulisimamia kuliko yule unayemwandikia,ila yote katika yote pamoja sana Ncha Kali 🤝🤝
 
View attachment 2291152
View attachment 2291153
Jamii Forums, Asasi ya Kiraia inayohamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora na mratibu wa jukwaa la mtandaoni la JamiiForums.com (JF), imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (Citizen Journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi na wananchi wenzao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai.

Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye awamu nyingine ya shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko chanya (Stories of Change).

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Awamu hii ya pili ya shindano hili itafanyika Julai 15 hadi Septemba 14, 2022.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  1. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
  2. Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
  3. Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
  4. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
  5. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  6. Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.

Jinsi ya kushiriki:

Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili.

Maandiko yawasilishwe kuanzia Julai 15 hadi Septemba 14, 2022 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )

Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.

ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Vigezo vya kupata Washindi
Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura/likes zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (30%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (70%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo.

Ni muhimu kuendelea kuwa ‘active’ katika jukwaa la JF muda wote wa shindano ili kurahisisha mawasiliano endapo utaibuka mshindi.

Zawadi kwa Washindi
Mshindi wa Kwanza Tsh. 5,000,000
Mshindi wa Pili Tsh. 3,000,000
Mshindi wa Tatu Tsh. 2,000,000
Mshindi wa Nne Tsh. 1,000,000
Mshindi wa Tano Tsh. 500,000
Mshindi wa Sita hadi kumi Tsh. 300,000
Mshindi wa Kumi na Moja hadi wa Ishirini Tsh. 200,000

Mawasiliano

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
Woooow golden chance to everyone
 
Title na kuondolewa vinahusianaje sasa tunachohitaji kujua ni Kwa Nini zinaondolewa na wakati wanahitaji zipigiwe kura....Confusion🤔🤔!!!!!!
maana aliandika nyingi nilitaka nizijue zilizofutwa tu.
 
Back
Top Bottom