Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png

Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Bado changamoto ya kupiga kura kwa wenye App haijatatuliwa, inaweza kuwa bora wapiga kura wakashauriwa kutumia web wakati JF mnaendelea kutatua hiyo changamoto.
 
Habari leo Rais mwenyekiti wa baraza la mawaziri ya mapinduzi , Ali Hassan mwinyi leo ametengua uteuzi wa ukurugenzi wa idara ya nyaraka ya kumbukumbu ya zanzibar, Salum suleimani salum ,
 
Mahakama ya kisutu : mahaka ya mkazi ya kisutu imefutia kesi ya dereva wa taski hakimu kumuachia uhuru alikuwa akiitwa kwa jina ya mousa twaleb alishitakiwa kwa kumteka mfanyabiashara maarufu mohamed Dewji
 
Rais wa tunisia kais saied amesitisha shughuli zote za bunge pamoja na kufuta kazi za waziri mkuu wa nchi hiyo mw. Hechim mechichi kufuatia maandamano ya wananchi waliolaumu chama kilicho madarakani
 
Chadema imedai kuwa mwenye kiti wao freeman mbowe amefikishwa mahakama ya kisutu kwa kesi ya kusomewa shitaka la ugaidi na kupelekwa gerezani
 
View attachment 1850745

Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 15, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 15, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
Mimi naandika kitabu cha ujasiriamali ambacho kimebeba mengi ya hayo na kiko kwenye hatua za mwisho naimeandika kwa lugha ya kiingereza
 
Mkuu Maxence Melo naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Pamoja na kwamba mtu unapaswa kuandika wazo lako binafisi, je, naruhusiwa ku refer kwa ajili ya kukoleza au kukomelea fact au takwimu nitakayokuwa labda nimeitoa kwenye andiko langu? Asante.
 
Haya mkuu, ungepunguza maneno lakini,kwa anayetaka hata aende beyond 3,000 words ni sawa,ila kwa wengi waandike maneno yasiyozidi 300, itasaidia kubaki kwenye objectivity, lengo la shindano ni kuisaidia jamii yetu,itakuwa vibaya kama jamii haitaona huo msaada,namaanisha long essays/topics siku zote humu huwa zina muitikio hafifu/ignored.

Na hivyo kwenye hili shindano watu hawavote kabisaa sababu kusoma topic yote hawajasoma kwa sababu ni ndefu. mtu akishaona ndefu anaenda next one and next one without voting. Shindano ili kuifikia jamii yetu ni lazima tuwe short and precise, sio inasaidia voting peke yake but sending key message kwa jamii kwa ujumla
Hilo halitakuwa shindano kwa haya unayoweka hapa!
 
Mbali na kuwasogeza Watanzania karibu kuhoji, kukosoa, kuonya na kushauri juu ya rasilimali na mienendo ya umma kwa maslahi mapana ya Taifa lao, Bado hamkuwaacha nyuma katika suala la uwajibikaji na fursa.

Mbarikiwe JamiiForums
 
Mkuu Maxence Melo naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Pamoja na kwamba mtu unapaswa kuandika wazo lako binafisi, je, naruhusiwa ku refer kwa ajili ya kukoleza au kukomelea fact au takwimu nitakayokuwa labda nimeitoa kwenye andiko langu? Asante.

Sina uhakika lakini nafikiri inaruhusiwa kufanya rejea kukazia wazo lako. Mfano kuna vitu kama takwimu, picha na baadhi ya taarifa muhimu ambazo zinapatikana kutoka vyanzo maalum, unaweza kuvitumia ilimradi uonyeshe chanzo.

Kikubwa wazo au maudhui mazima ya chapisho lako iwe ni wazo lako.
Hayo ni mawazo yangu lakini watakuja JF kutoa muongozo.
 
Msaada anayeweza kuscreenshot kipande kinachoonesha sehemu ya kupigia kura kwenye hili shindano.
Maana wengine bado hatujajua,tunashindwa kupiga kura
 
Sina uhakika lakini nafikiri inaruhusiwa kufanya rejea kukazia wazo lako. Mfano kuna vitu kama takwimu, picha na baadhi ya taarifa muhimu ambazo zinapatikana kutoka vyanzo maalum, unaweza kuvitumia ilimradi uonyeshe chanzo.

Kikubwa wazo au maudhui mazima ya chapisho lako iwe ni wazo lako.
Hayo ni mawazo yangu lakini watakuja JF kutoa muongozo.
Asante sana kwa ufafanuzi mujarabu mkuu. Ngoja tuwasubiri wenyewe waje.
 
Wakuu Maxence Melo and Admin1988 naombamnisaidie kutatua hii changamoto. Nataka kumpigia mtu kura kwenye stories of change lakini sipati option ya kupiga kura kama inavyoonekana hapa chini. please assist.
1627403695566.png
 
View attachment 1870588
Kwa hii screenshot, ni wazi upo via PC.

Angalia PEMBENI mwa mjadala husika (1st post) utaona sehemu imeandikwa VOTES) ndipo ubonyeze mshale wa kwenda juu.

Screenshot 2021-07-27 at 19.48.50.png
 
Back
Top Bottom