Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
1F70230F-13AA-4521-B56F-33278A4DC9F4.png

Jamii Forums (JF) ni Asasi ya Kiraia inayoratibu mtandao wa JamiiForums na kuhamasisha Haki za Kidigitali, Demokrasia, Uwajibikaji na Utawala Bora.

Jamii Forums imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uandishi wa maudhui bora na yenye tija mtandaoni kwa zaidi ya miaka 15 kwa kutoa jukwaa la umma kwa wananchi (citizen journalists) kujieleza bila uoga, kuwawajibisha viongozi wao na kujenga uelewa zaidi katika masuala anuai. Ni kupitia safari hii na kujitolea kwake kwa Utetezi wa Haki za Dijitali, Jamii Forums inaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuhakikisha mtandao unabaki mahali salama ambapo umma wa Watanzania unaweza kupata habari/taarifa bora na pia kutengeneza maudhui yanayochochea mabadiliko chanya.

Hivyo basi, JF inatoa nafasi kwa wadau wake na wananchi wote wenye uwezo wa kutayarisha maudhui kushiriki kwenye mashindano ya uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta mabadiliko(Stories of Change).

Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 30, 2021.

Shindano hili linakusudia kuongeza maudhui bora mtandaoni hususani ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Pia, tunalenga kuhamasisha ushiriki wa raia pamoja na makundi yasiyopewa vipaumbele kama watu wanaoishi na ulemavu kushiriki katika ukusanyaji na utayarishaji wa taarifa nchini.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:

  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Uchumi na Biashara, Afya, Maendeleo ya Jamii, Utawala Bora na Uwajibikaji, Demokrasia, Kilimo, Sayansi na Teknolojia, Haki za Binadamu n.k.
  • Andiko linaweza kuwa la Kiswahili au Kiingereza lenye maneno yasiyozidi 1,500.
  • Mshiriki atapewa saa 2 tu kulihariri andiko lake baada ya kulichapisha jukwaani hivyo atatakiwa kuwa makini katika uwasilishaji wake
  • Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili
  • Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa ushirikiano endapo ataibuka mshindi
  • Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism haitaruhusiwa
  • Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki atalazimika kutaja chanzo
Jinsi ya kushiriki:
  • Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kushiriki, lakini ili kuchapisha Makala yako itakulazimu kuwa mwanachama wa JamiiForums. Endapo sio mwanachama unaweza kujisajili kupitia => (www.jamiiforums.com/register/ ). Ukipata changamoto katika usajili, wasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyowekwa chini katika bandiko hili
  • Maandiko yawasilishwe kati ya Julai 14 – Septemba 30, 2021 kwenye jukwaa la “JF stories of change” (Stories of Change )
  • Baada ya kuweka andiko lako jukwaani, JITAHIDI kushiriki kwenye mjadala utakaotokana nalo kwa kutolea ufafanuzi hoja zitakazoibuka ili kuupa mjadala uhai na kuwashawishi wanachama kukupigia kura.
ZINGATIA: Unaweza kuandika mara nyingi kadiri uwezavyo ili kujiongezea nafasi ya ushindi.

Zawadi kwa Washindi

Washindi watapatikana kwa kuzingatia kura zitakazopigwa kwenye mnakasha (thread) husika (40%) na pia uamuzi wa jopo la majaji (60%).

Washindi watatangazwa kwenye jukwaa la JamiiForums “Stories of Change” na kurasa za Jamii Forums katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Instagram na Telegram) na si vinginevyo

Zawadi kwa Washindi zitakuwa kama ifuatavyo:-

Mshindi wa Kwanza atapata fedha taslimu shilingi Milioni 5
Mshindi wa Pili atapata fedha taslimu shilingi Milioni 3
Mshindi wa Tatu atapata fedha taslimu shilingi Milioni 2

Zawadi nyingine zitahusisha Laptop, Tablet na Simu za mkononi.

Mawasiliano
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya simu: +255 743440000 (WhatsApp, Telegram na Signal) au barua pepe: stories@jamiiforums.com
 
Upvote 0
Kulikua na tatizo la watu kushindwa kupiga kura kwa wanaotumia app, sijui kama lilishatafutiwa ufumbuzi.

Vinginevyo, ni mwanzo mzuri kwa JF kugusa jamii kwa namna tofauti. Hongereni sana.
 
SIRI YA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.

mafanikio.ni riziki ama malengo unayoyafikia baada ya kufanya jambo lolote katika utafutaji maishani mwako na hayo mafanikio yanaweza kugusa nyanja zote za maisha kama vile kiuchumi,kijamii,kiutamadani n.k

HOJA ZA KUKUSAIDIA UFANIKIWE MAISHANI NI HIZI HAPA:
1.Elimu
2.ajira
3.mtaji
4.fursa
5.nguvu kazi
6.ujuzi na ubuunifu
7.kutokata tamaa
8.nidhamu katika kazi

1.ELIMU
Ukihitaji kufanikiwa na kuendana na sayansi na technolojia ya sasa unahitaji kupata elimu ili uweze kuendana na kasi ya utafutaji pia elimu itasaidia kujifunza namna mbali mbali za utafutaji na fursa kadha wa kadha na hiyo pia upande wa serikali inatakiwa kuanzisha elimu maalumu ambazo zitatolewa kwa kulenga kazi ama fursa husika kwa maana kuanzisha mitaala ambayo itakuwa rafiki na yenye manufaa kwa watakao somea ,hivyo elimu ni jambo la msingi na muhimu sana unapohitaji kubadirika.

2.AJIRA.
hili pia na jambo la muhimu sana ili jamii iweze kubadilika kimaendeleo na kupiga hatua kimaisha hapa tunalenga serikali mojakwamoja inatakiwa itengeneze ajira ama kazi tofauti tofauti ambapo wale walio pata elimu za kada mbalimbali waweze kupata ajira kutoka serikalini pia serikali inajukumu la kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kuongeza wigo mpana wa kuwepo kwa ajira nyingi zaidi ,na kwa wale ambao hawaja soma pia wanahitaji kujiajiri kwa sababu wanauwezo kuendesha shughuli mbalimbali mfano ujasiriamali hivyo ajira ndio kila kitu bila hivyo mtu aujamii haiwezi kubadilika hivyo ni jambo la msingi sana
 
Hizo Nondo hawaandiki hapa.
Nenda jukwaa la stories of change ndipo utiririke.
 
Ni wazo zuri kabisa. Ila kama mshindi atapatikana kwa kupigiwa kura; basi rikiboy na maudhui yake 'kimasihara' atashinda asubuhi.

Jamii ya Watanzania inapenda zaidi burudani na mizaha kuliko mijadala na maudhui serious.

Mkuu UMESEMA UKWELI KABISA
 
Mpeni malila tu

He is a hero

Sijui hata Yuko wapi these days
Habari wanajamvi.
Namshukuru Mungu nipo hai, bado naendelea na kupiga kazi kwa nguvu zaidi. Asante kwa kunikumbuka mkuu.
 
Back
Top Bottom