Shinikizo laongezeka dhidi ya serikali ya Ethiopia kuhusu jimbo la Tigray

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Marekani yasema itaiwekea vikwazo Ethiopia baada ya serikali ya nchi hiyo kuwafukuza maafisa saba wa mashirika ya kutoa misaada ya Umoja wa Mataifa ambao wanadaiwa kujihusisha na maswala ya ndani ya nchi hiyo.

Symbolbild I UN I Äthiopien

Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imewapa maafisa saba wa Umoja wa Mataifa muda wa saa 72 kuondoka Ethiopia kwa kile ambacho serikali ya nchi hiyo imedai wamejiingiza katika mambo ya ndani ya ya nchi hiyo. Wakati huo huo shinikizo linaongezeka dhidi ya serikali ya Ethiopia kuhusu jimbo la Tigray.

Serikali ya Ethiopia imechukua uamuzi wa kuwafukuza maafisa hao wa Umoja wa Mataifa baada ya wafanyakazi wa kutoa misaada kutanabahisha juu ya hali ya maafa katika jimbo la Tigray inayotokana na kushindikana kupeleka misaada kwenye sehemu hiyo. Miongoni mwa maafisa hao saba wa mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa wanoatakiwa kuondoka nchini Ethiopia ni pamoja na naibu mratibu wa misaada nchini humo Grant Leaty na mwakilishi wa shirika la watoto la UNICEF, Adele Khodr.

Mwakilishi wa UNICEF Adele Khodr
Mwakilishi wa UNICEF Adele Khodr

Umoja wa Mataifa umesema hatua ya kuwafukuza maafisa wake kutoka nchini Ethiopia inahatarisha zaidi ufikishaji wa misaada ya kibinadamu katika mkoa wa Tigray ulio na watu wapatao milioni 6 na unaokumbwa na mgogoro kwa karibu mwaka mmoja sasa. Umoja wa Mataifa umesema shughuli za kupeleka vifaa vya matibabu, chakula na mafuta zimesimama.

Msemaji msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephanie Tremblay, amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuziangazia shida zinazowakabili watu wa jimbo la Tigray.

Serikali ya Ethiopia imewashutumu wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa kwa kuunga mkono vikosi vya Tigray ambavyo vimekuwa vikipambana na wanajeshi wa serikali ya shirikisho na vikosi vya washirika wake tangu mwezi Novemba mwaka uliopita. Wafanyikazi hao wamekana shutuma hizo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada, Martin Griffiths, wiki hii aliliambia shirika la habari la The Associated Press (AP) kwamba mgogoro nchini Ethiopia ni doa kwa dhamira ya ubinadamu kwa kuwa watoto na watu wengine wanakufa kwa njaa katika jimbo la Tigray kutokana na serikali kuzuia misaada. Watu wapatao 400,000 wanakabiliwa na hali mbaya ya njaa.
 
... mlokole Abiy alianza vizuri sana kama msabato Hichilema na Nobel juu (Abiy) ila anaharibu sasa!
 
Ndg Ethiopia ni ngumu sana kuiongoza...Ni style zile zile za Uarabuni bila mkono wa chuma hapo hapatawaliki...Nionyeshe Libya Iko wapi bila mtiti wa Gadafi imeishaa.

Kila Mtu ni mbabe...Kuna Ujinga sana Pale Ethiopia hawa Tigray wanataka wao watawale nchi na ndio matajiri wengi.

Wameumiza sana Wenzao kwa miaka sasa wanaumia roho wanaona wajitenge...Tigray Yenyewe ni eneo kubwa kweli na lina watu wengi watu mil 7.

Ni Kama Nchi ndani ya Nchi...Wengi Wao Wasomi na Matajiri wakubwa...
 
Hawa Ethiopia enzi za magufuli wanaharakati wa twita wakiongozwa na dada yao ndio walikuwa wanawasifu kuwa vinara wa demokrasia. Naona pm wao anaendelea kuupiga mwingi.
 
Ndg Ethiopia ni ngumu sana kuiongoza...Ni style zile zile za Uarabuni bila mkono wa chuma hapo hapatawaliki...Nionyeshe Libya Iko wapi bila mtiti wa Gadafi imeishaa.

Kila Mtu ni mbabe...Kuna Ujinga sana Pale Ethiopia hawa Tigray wanataka wao watawale nchi na ndio matajiri wengi.

Wameumiza sana Wenzao kwa miaka sasa wanaumia roho wanaona wajitenge...Tigray Yenyewe ni eneo kubwa kweli na lina watu wengi watu mil 7.

Ni Kama Nchi ndani ya Nchi...Wengi Wao Wasomi na Matajiri wakubwa...
Wawaruhusu wajitenge,shida iko wapi?
 
Chadema walikuwa wanataka serikali ya majimbo, unaona madhara yake kwa serikali za kiafrika au Uarabuni. Yaani unakuwa na serikali ndani ya serikali kila jimbo, huku ni Afrika au Uarabuni, haya mambo hayawezekaniki. Serikali ya Jimbo la Tigray limekuwa na nguvu kubwa sasa linapigana na serikali kuu ya Ethiopia. Waafrika au waarab huwezi tawala kwa demokrasia ya hivyo, ubabe ndio njia pekee ya kutawala Afrika au Uarabuni.
 
... mlokole Abiy alianza vizuri sana kama msabato Hichilema na Nobel juu (Abiy) ila anaharibu sasa!
Ile tuzo ya nobel alipewa kisiasa tu (kama alivyopewa Obama) ila Sasa ndio kaonyesha rangi yake halisi.
 
Chadema walikuwa wanataka serikali ya majimbo, unaona madhara yake kwa serikali za kiafrika au Uarabuni. Yaani unakuwa na serikali ndani ya serikali kila jimbo, huku ni Afrika au Uarabuni, haya mambo hayawezekaniki. Serikali ya Jimbo la Tigray limekuwa na nguvu kubwa sasa linapigana na serikali kuu ya Ethiopia. Waafrika au waarab huwezi tawala kwa demokrasia ya hivyo, ubabe ndio njia pekee ya kutawala Afrika au Uarabuni.
Tatizo la Ethiopia ni zaidi ya serikali ya majimbo, nenda kajisomee vizuri.

Isitoshe hata Nigeria wana serikali ya majimbo ila udini, ukabila,ufisadi na Sasa ugaidi unaitafuna...serikali ya majimbo sio kikwazo kwa maendeleo ya nchi hata mataifa makubwa yenye maendeleo kama India,Urusi, Marekani,Ujerumani yana serikali za majimbo.
 
Ile tuzo ya nobel alipewa kisiasa tu (kama alivyopewa Obama) ila Sasa ndio kaonyesha rangi yake halisi.
Does it mean kamati ya nobel haikuwa makini? Au ndio hivyo tuzo yenyewe imeanza kupoteza maana yake iliyokusudiwa toka mwanzo?
 
Walimpa hiyo tuzo baada ya kusaini makubaliano ya amani na nchi jirani na hasimu wao mkubwa (Eritrea), hii ilikuwa kabla ya mgogoro kati yake na Chama na Tplf.

Ila baada ya mgogoro kati yake na Chama Tplf kuzuka cha kushangaza aliungana na hasimu wake huyo wa zamani (jeshi la Eritrea) kushambulia raia wa nchi yake mwenyewe huko Tigray.

Tatizo sio kupewa tuzo ila nadhani wengi wakishapewa hii tuzo wanadhani wamepewa ruhusa ya kufanya watakalo maana wameaminiwa na wakubwa wa dunia.

Ni vyema hii tuzo wapewe viongozi waliostaafu.
 
...

... shukrani Chief kwa ufafanuzi. Kwa uapande wa viongozi kama ulivyosema kama ni lazima sana itolewe kwa viongozi wa kisiasa basi wawe na retired with outstanding performance haswa otherwise non-political personalities ambao mchango wao kwa dunia hauna chembe ya mashaka.
 
Walimpa hiyo tuzo baada ya kusaini makubaliano ya amani na nchi jirani na hasimu wao mkubwa (Eritrea), hii ilikuwa kabla ya mgogoro kati yake na Chama na Tplf.

Ila baada ya mgogoro kati yake na Chama Tplf kuzuka cha kushangaza aliungana na hasimu wake huyo wa zamani (jeshi la Eritrea) kushambulia raia wa nchi yake mwenyewe huko Tigray.

Tatizo sio kupewa tuzo ila nadhani wengi wakishapewa hii tuzo wanadhani wamepewa ruhusa ya kufanya watakalo maana wameaminiwa na wakubwa wa dunia.

Ni vyema hii tuzo wapewe viongozi waliostaafu.
Unaweza kutupa analysis yako kama ungekuwa PM wa Ethiopia ungefanyaje?
Maana kuna mambo ni rahisi sana kuyasema kuliko kuyaishi!
Huyu PM amekuwa muungwana sana. Hii scenario angekuwa Qaddafi au Mugabe au watu wa aina hii ndio ungeusoma mchezo vizuri!
 
Huyo PM kaharibu nchi yake....kafeli vibaya.

Hao kina Qaddafi na Mugabe mwisho wa ubabe wao umekuwa aibu na fedhea tu, sio mifano mzuri kabisa.
 
Okay sawa, tupe basi analysis yako. Ungekuwa ndio mr. PM na situation ndio imefikia pale, ungefanyaje? Ili angalau tuone kama kweliuna better alternative
 
Ukifahamu sababu ya Abiy kuanzisha vita na hao Watigray utagundua njia ya mazungumzo ndio suluhisho bora kwa pande zote.
 
Unamaanisha angeanzisha mazungumzo na watu waliokuwa wameanza kushambulia kambi za Federal army? Hayo mazungumzo yanakuwaje?
 
Tatizo la Ethiopia ni zaidi ya serikali ya majimbo, nenda kajisomee vizuri.

Isitoshe hata Nigeria wana serikali ya majimbo ila udini, ukabila,ufisadi na Sasa ugaidi unaitafuna...serikali ya majimbo sio kikwazo kwa maendeleo ya nchi hata mataifa makubwa yenye maendeleo kama India,Urusi, Marekani,Ujerumani yana serikali za majimbo.
Serikali ya majimbo ni tatizo, hayo mataifa unayosema yako imara kwasababu ya ukongwe wake, ila kwa mataifa machanga kama haya yetu huo mfumo haifai, mfumo bora ni huu wetu wa mikoa

Kiongozi wa mkoa ni mteule wa mkuu wa nchi, na ndio mkuu wa usalama wa mkoa husika,
Hutakaa usikie mkuu wa mkoa anaongoza mapinduzi ya mkoa kujitenga

Ila Ethiopia hilo ndilo l inatokea kwasababu mkuu wa jimbo anapatikana kwa kura
 
Lengo la serikali ya majimbo ni kushusha madaraka mpaka mikoani, hiyo hofu ya kujitenga mnaitoa wapi?

Kwanini mnampa kiongozi wa nchi mamlaka makubwa ya kuwateulia watu kiongozi wa mkoa ilihali raia wa eneo hilo wanaweza kufanya hilo?

Isitoshe hayo majimbo yanabaki na madaraka ya ndani tu ila taasisi muhimu kama ulinzi (majeshi), mambo ya nje, zinabaki mikononi mwa serikali kuu.
 
Back
Top Bottom