Shinyanga: Bweni la Shule ya Msingi Buhangija lateketea kwa moto na kuua wanafunzi watatu

Shinyanga: Bweni la Shule ya Msingi Buhangija lateketea kwa moto na kuua wanafunzi watatu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Wanafunzi watatu wa shule ya msingi Buhangija na kituo cha elimu maalumu Buhangija Manispaa ya Shinyanga wamepoteza maisha, baada ya bweni la wasichana walilokuwa wamelala kuungua moto usiku wa kuamkia leo huku wengine wakinusurika baada ya kuokolewa

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amethibitisha kutokea tukio hilo ambapo amesema moto huo umeanza kuwaka majira ya saa tano usiku wakati wanafunzi 32 wakiwa wamelala ndani ya bweni hilo

bweni.png
 
Pole kwa wazazi waliofikwa na Msiba huo poleni sana na Mungu awatie nguvu kwa kipindi hiki mnachopitia.
 
Bora mtoto asome day tu.Hizi za kulala usalama umekuwa changamoto sana
 
Tukio limetokea katika Shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga baada ya bweni walilokuwa wamelala wanafunzi hao kuteketea kwa moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa, Janeth Magomi amesema moto ulioteketeza bweni la wasichana ulizuka saa 5 usiku wa kuamkia Novemba 24, 2022.

Magomi amesema Jeshi hilo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto.

========================

Wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga wamefariki dunia huku 29 wakinusirika baada ya bweni walilokuwa wamelala kuteketea kwa moto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea tukio hilo huku akisema moto huo uliyoteketeza bweni la wasichana la shule hiyo umezuka saa 5 usiku wa jana Jumatano, Novemba 24, 2022.

"Moto huo umeanza kuwaka usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wamelala ndani ya bweni ambapo idadi yao walikuwa 32 waliokuwa ndani wengine wameokolewa," amesema Magomi

Magomi amesema maofisa wa Jeshi hilo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

MWANANCHI
 
Matamko makali yanayotolewa baada ya matukio hatari kutokea zinahuzunisha wananchi.

Uchakavu wa mabweni, kuweka Vidhibiti moto kwa majengo wanapoishi hao watoto wasiojiweza, mwangalizi wa zamu wa watoto hao, nk ni ishara tosha kuwa viongozi wa ngazi zote wanaongoza kwa mazoea.

Ajali kama hii kuna haja Gani ya kuunda bodi ya uchunguzi? Majengo yote ya shule yalipo nje ya mkoa wa Shinyanga yamechakaa sana kwa sababu yalijengwa kwa matofali ya mfinyanzi.

Mfano Itilima SM Wilaya ya Kishapu Km 30 kutoka Shinyanga mjini Hali yake inasikitisha sana. Mama Samia ametoa mabilioni ya shilingi kujenga shule fedha zaenda wapi?

IMG_20221122_152803_598.jpg
IMG_20221122_153218_723.jpg
 
Hizo bodi za uchunguzi kuhusu majanga hayo yanahararisha nini?Jana mjumbe kamati ya shule alitamka kuwa majengo ni chakavu na kuna jengo jipya limeishakamilika kwa matumizi ya bweni.Sasa lawama ni kwa nani? Kuna dhahama nyingine inaonekana kwenye picha watoto wansomea kwenye jengo bovu je wakifunikwa na kifusi mtafanya uchunguzi,?
 
Shule ya watu wenye mahitaji maalum lakini hakuna automatic fire extinguisher?
 
Back
Top Bottom