JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Harold Gamalieli Mkaro ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Makedonia Lubaga Manispaa ya Shinyanga amesomewa shtaka la kujaribu kulawiti mtoto wa miaka 6 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga.
Agosti 24, 2022 Mchungaji huyo alifutiwa kesi namba 107 na Jamhuri katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga kwa sababu za kisheria ambapo alikamatwa tena na kurejeshwa mahabusu alikokaa kwa siku 5 hadi Agosti 29, 2022 alipofikishwa Mahakamani kwa mara nyingine.
Mshtakiwa amekana shitaka hilo analodaiwa kulitenda Agosti 8, 2022. Upelelezi umekamilika, mshtakiwa alikwama kupata dhamana kutokana na mmoja wa watu wake kutokidhi vigezo, hivyo akarejeshwa rumande.
Kesi hiyo itaendelea leo Agosti 30, 2022 kwa Mahakama kuanza kuwasikiliza mashahidi 6.