Shinyanga: Mume aua mkewe na kisha kujilipua ndani ya nyumba kwa Petroli baada ya Wazazi wake kuvunja Ndoa yao

Shinyanga: Mume aua mkewe na kisha kujilipua ndani ya nyumba kwa Petroli baada ya Wazazi wake kuvunja Ndoa yao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wenslausi James (30) na Betha Kasimili (25), ambao ni wakazi wa kijiji cha Busongo kata ya Mwamashele wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, wamefariki dunia baada ya mwanaume huyo kujilipua kwa moto kwa kutumia mafuta ya Petroli, kwa madai ya wazazi wa mwanaume kumkataa mwanamke.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, Kamishina msaidizi wa Polisi, Jackson Mwakagonda, tukio hilo limetokea June 14 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi.

Mwakagonda amesema wanandoa hao walikuwa wamezaa watoto watatu, lakini wazazi wa mwanaume walimkataa mke wake, na kuamua kuuvunja mji pamoja na kurudisha mahari nyumbani kwao na mwanamke.

Aidha, amesema baada ya mji huo kuvunjika, ndipo mwanaume akasikia kuwa mke wake anataka kuolewa, na kuamua kwenda nyumbani kwa kina mwanamke akiwa na dumu la mafuta ya Petroli lita tano, na kisha kuingia chumbani kwa mwanamke na kufunga mlango na kisha kuanza kugombana.

“Mwanaume huyu alimchoma kisu cha ubavuni mke wake, na kisha kumfunga minyororo na kumwagia mafuta ya Petroli, kisha na yeye kujimwagia Petroli akawasha kiberiti na kujilipua moto, ambapo waliteketea pamoja na nyumba,” amesema Mwakagonda.

Aidha Kamanda ametoa wito kwa wazazi, kuacha kuingilia ndoa za watoto wao, pamoja na wanandoa kuacha kujichukulia sheria Mkononi, na pale penye migogoro bali watafute ufumbuzi kwa kufuata sheria.

Chanzo: Dar24
 
Huyo jamaa Wenslaus James qmlmmyk kabisa yeye na wazazi wake! Yaani pimbi ameenda kumuua mke wake kikatili na kuunguza nyumba ya wakwe zake kwa kosa lipi hasa? Yeye hakuona kosa lilianzia kwa wazazi wake mwenyewe (baba + mama Wenslaus) kumkataa 'mkamwana' wao? Kwanini hakwenda kuwachoma wazazi wake? Jamaa kenge wa pinki kabisa huyo.

Halafu jambo jingine,Mwanaume mzima utachukuaje maamuzi ya kipumbavu hivi? Unaua na kujiua kwasababu ya keys*nge namna hii? Yaani kuna brother'angu ana kansa inamtesa kinyama,mke amemkimbia,mali zake zimeuzwa ili kugharamia matibabu,mwaka jana akashindwa kesi ya madai mahakamani yet jamaa is still full of hope,anatutia moyo,hajasurrender na hajawahi kifikiria kujiua.Kwanini yeye Wenslaus afanye hivyo?

Yaani hapa nina hasira na huyo nguruwe utadhani mimi ndo baba mkwe wake au shemeji yake (kaka wa Bertha Kasimili).

HIVI SIKU HIZI WANAUME HATUWEZI KABISA KUHIMILI CHANGAMOTO ZA MAISHA? WHAT'S OUR MANHOOD THEN?
 
HIVI SIKU HIZI WANAUME HATUWEZI KABISA KUHIMILI CHANGAMOTO ZA MAISHA? WHAT'S OUR MANHOOD THEN?
this is very good point.... kuna tatizo tunalo sisi wanaume wa kizazi hiki...hili suala ni lazima liwe addressed haraka sana kabla mambo hayajazidi kuharibika. " Uanaume wetu tuliopewa na Muumba umekwenda wapi? "
 
Wazazi wa miaka hii wanakuwaga na mambo ya ajabu sana muda mwingine. Sikatai inawezekana kuwa mzazi ana nia nzuri ya kumlinda mtoto wake ila sasa kwann uingilie kwa namna unataka wewe why usikae na hao vijana uwaelezee doubts zako.

Watu wamependana wewe mzazi unaanza kuleta maneno ya chini chini kuharibu ndoa ambayo wao wanaona haina shida.

Na jambo jingine ni maamuzi ya kukurupuka bila kujali hisia za mwingine. Yaani mtu anaamua kwa kichwa chake pekee yake kuwa nitafanya hivi hata kama fulani ataumia mimi still nitafanya tu bado.
Hii ni aina ya psychological attack kwa mtu ambaye hajajiandaa kupokea maamuzi ya hivyo. Unaweza shangaa mtu kafanya maamuzi kama kichaa kisababishi ni mshtuko wa kisaikolojia. Ni vema kufanya maamuzi ambayo ndani yake yana consideration ya wote na sio mtu m'moja anae amua.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom