Shinyanga: Wajaziwa maji kwenye magari badala ya mafuta

Shinyanga: Wajaziwa maji kwenye magari badala ya mafuta

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Baadhi ya watu wamedai kujaziwa mafuta kwenye magari yao ambayo yana maji kwenye kituo cha mafuta cha Total energies Shinyanga na walipomfuata meneja wa kituo hakuwapa majibu mazuri,

Hata hivyo, jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga limesema kuwa wanafanya uchunguzi ambapo watawashirikisha EWURA na wao watahusika ili kujua iwapo injini zimeharibika na magari yanawaka au lah ikiwemo na mambo mengine ya kiuchunguzi.



==================
​
Wamiliki wa magari Mjini Shinyanga wamelalamikia kujaziwa maji badala ya mafuta katika moja ya kituo cha mafuta mjini humo, hali iliyosababisha magari yao kushindwa kuwaka.

Tukio hilo limetokea Aprili 7, 2026 majira ya saa 7 hadi 8 mchana, ambapo baadhi ya wateja walijikuta wakikumbwa na hitilafu mara baada ya kujaza mafuta na kuanza safari zao.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamesema walishuhudia magari yakimwaga maji kutoka kwenye mifumo ya mafuta, huku kukiwa na mzozo mkali kati ya meneja wa sheli hiyo na wamiliki wa magari walioathirika.

Mmoja wa waathirika, Yona Limo, amesema baada ya kujaza mafuta na kuanza safari, gari lake lilianza kuonyesha hitilafu, hali iliyomlazimu kwenda gereji ambapo ilibainika kuwa alikuwa amewekewa maji badala ya mafuta.

“Niliporudi kulalamika, nilikuta magari mengine nayo yakirudi, wamiliki wakidai wamewekewa maji badala ya mafuta,” amesema Limo.

Naye Adamu Richard, aliyekuwa akisafiri kuelekea Kahama, amesema gari lake pia lilipata hitilafu muda mfupi baada ya kujaza mafuta katika sheli hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa tayari watu wanne walikuwa wamewasilisha malalamiko rasmi kwa Jeshi la Polisi.

Amesema uchunguzi wa kina unaendelea kwa kushirikiana na EWURA ili kubaini ukweli wa tukio hilo, huku magari yaliyoathirika yakitarajiwa kufanyiwa uchunguzi na kikosi cha usalama barabarani.

Kwa sasa, sheli hiyo ipo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi hadi uchunguzi utakapokamilika na hatua za kisheria kuchukuliwa.
 
Back
Top Bottom