Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
Habari wanajamvi,

Natumaini mu wazima na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku. Nimekuja kwenu leo nikiwa na swali ambalo ningeomba msaada wenu kulijibu. Katika kutafuta bima ya afya ambayo itakuwa na gharama nafuu na huduma bora, nimepata majina ya mashirika kadhaa yanayotoa huduma za bima ya afya Tanzania. Haya ni baadhi ya mashirika:

  1. NHIF (National Health Insurance Fund)
  2. AAR Insurance Tanzania
  3. Jubilee Insurance
  4. Strategis Insurance Tanzania
  5. Britam Insurance Tanzania
  6. First Assurance Tanzania
  7. UAP Insurance Tanzania
  8. Sanlam Life Insurance Tanzania
  9. Alliance Insurance Corporation Ltd
  10. Phoenix of Tanzania Assurance Company Ltd
  11. Metropolitan Tanzania Insurance Company

Nipo kuchanganua Bima yenye gharama nafuu, hasa kwa haya mashirika ya Bima kwa mwaka kwa mtu mmoja au kwa mtoto bima zao zikoje najua NHIF imepandisha gharama kwa haya mashirika mengine nayo hakuna yenye nafuu kuzidi NHIF?

Ningeomba msaada wenu katika kufahamu ni shirika gani kati ya haya linaweza kuwa na gharama nafuu na kutoa huduma nzuri. Kama una uzoefu na mojawapo ya mashirika haya au unajua lolote kuhusu vifurushi vyao vya bima ya afya, tafadhali shiriki maoni yako.

Pia, ningependa kujua:

1. Je, kuna kifurushi chochote cha bima ya afya kutoka mojawapo ya mashirika haya ambacho kina gharama nafuu kwa mtu mmoja au wawili kwa mwaka?

2. Kati ya mashirika haya, ni lipi lina huduma bora zaidi kwa wateja wake?

3. Kuna shirika lingine lolote ambalo unalipendekeza kwa gharama na huduma bora?

Maoni yako ni muhimu yanaweza kusaidia hata ambae hakuwa na nia ya kuhitaji Bima akashawishika hapa baada ya kusoma maoni hapa.

Karibuni kwa majadiliano!
 
Kwa bei vs huduma…. NHIF Bado Haina mpinzani

Hayo mengine ni very expensive,, hayapigiwi kelele because ni private

Ni tabia ya mtanzania kudharau public entities na kupapatikia private

NHIF Haina mpinzani
 
Kwa bei vs huduma…. NHIF Bado Haina mpinzani

Hayo mengine ni very expensive,, hayapigiwi kelele because ni private

Ni tabia ya mtanzania kudharau public entities na kupapatikia private

NHIF Haina mpinzani
Kwa hiyo gharama zao bado ni rafiki ukilinganisha na mashirika mengine?
 
Gharama nafuu huwa haziendani na huduma bora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…