The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Mimi ni mfanyakazi wa taasisi X ya umma hapa Shinyanga...
Nilichukua bima ya elimu (Education Provider With Profit) kwa ajili ya ada ya watoto wangu hapa tawi la NIC - Shinyanga yenye thamani ya Tshs 7,500,000 kwa makato ya Tshs. 62,500 kila mwezi kwa miaka kumi (10) tangu mwaka 2010...
Bima yangu imeiva tangu mwezi Oktoba mwaka huu 2020 na nimeshafuata taratibu zote kwa kuomba na kujaza papers zote zinazotakiwa ili kulipwa fedha zangu...
Surprisingly, huu sasa unaenda mwezi wa tatu silipwi pesa yangu. Kila nikifika kwenye ofisi zenu (NIC - Shinyanga) ni maneno tu badala ya kupewa fedha...
Kila mara mnasema faili langu bado liko makao makuu ya NIC - DSM, halijarudi ili kutoa "go ahead" ya kuandaliwa kwa malipo yangu...
That doesn't concern me please...!!
Basically haya ni majibu yenye maelezo ya ubabaishaji tu na hayana ukweli wowote...
Hivi ktk zama hizi za maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano na habari inawezekana vipi faili litembee lenyewe toka Shinyanga hadi DSM kwa miezi zaidi ya miwili pasipo kurudi....???
NIC - Shinyanga, tafadhali nikija safari hii naomba nikute fedha zangu na sitaki tuendelee kudanganyana kama watoto waliozaliwa Jana...
Ama la tuambieni mna matatizo gani?. Je, fedha zetu mliwapa CCM kufanyia kampeni za uchaguzi za mwaka huu kama mifuko ya hifadhi yq jamii (Provident Funds) walivyofanya na sasa wanawasumbua wazee wetu wastaafu kwa kutolipa mafao yao...?
NIC mnajichafua sana na kuharibu biashara yenu kwa sababu ya urasimu huu usio kuwa na ulazima wowote wa kushindwa kulipa fedha za wateja wenu wanaostahili kwa wakati...
Nilikuwa na mpango nikipata fedha hii, nikate bima nyingine lakini kwa usumbufu huu, bora niwekeze kihela changu ktk biashara nyingine....