Toka lini IMF wakatoa grants?
Siku zote world bank and IMF wanatoa Loan, maana ni taasisi za pesa zenye kufanya kazi zake kibenki zikipata faida kupitia riba. Tofauti ya hizi taasisi (IMF na World bank) na benki zingine za kibiashara iko kwenye riba na masharti. IMF na World bank wanakukopesha kwa riba nafuu na utalipa taratibu kwa muda mrefu lakini masharti yao ni mazito.
Wanaweza kukusamehe sehemu fulani ya deni wakiona huwezi kulilipa kwa wakati ili waweze kukukopesha tena.
Magufuli anajua kabisa kwa sasa hawezi kukopesheka kirahisi maana ana madeni makubwa, mwenendo wa kulipa unasusua na masharti ya kuweza kukopesheka hayawezi kuyatimiza ipasavyo.