Shirika la Ndege la Ethiopia limenifanya nateseka

Shirika la Ndege la Ethiopia limenifanya nateseka

Na kila wakiulizwa wanasema upo ethiopia wanautafuta nilikata tamaa zaidi Kwasababu NILIKATA JAMAA MWANASHERIA WA KAMPUNI INAITWA MROSO IPO DAR NA ARUSHA, AKANIAMBIA KWAKUWA SINA HELA ATANISAIDIA ILA ATADAI 100ML PAMOJA NA USUMBUFU, WANDUGU KWELI, SIKUWA TENA NA KITU ADI LEO JAMAA HAPOKEI SIMU YANGU
Pole sana mkuu

Hii ni mbaya, usiweke kichwa chini, haki haipotei ila itacheleweshwa, kwa bahati mbaya sana ukitumia muda na pesa kufukuzia hii haki kwa sasa utazama kabisa, ushauri wangu ni kwamba anza na biashara, na kila upatapo fursa fuatilia na shirika la ndege vya wanasheria wa hiyari sio hao commercial

kwa nilivyosikia, Mroso anapiga bei za juu sana
 
Pole sana ndugu yangu.
siku zote unatakiwa ujue kuwa bag la kuingia nalo ndani linatakiwa lisiwe kubwa sana kwa size na uzito kama 15kgs; Na ni vizuri lisiwe na vitu kama battery, vimiminika, mikasi, wembe nk.

kama begi lako ulirudishwa nalo mlangoni sina hakika kama liliweza kusajiliwa na kupewa luggage tag number? kwani kama hujapewa hiyo ref namba, mzigo huenda kuishia kwenye Godown ya hiyo ndege kama unidentified baggage.

-Kama bag lako lilipokelewa na ukapewa tag/ tag number; na ulipofika Bongo ukajaza lost luggage form kwa ref ya hiyo tag number ilikuwa rahisi kulifuatilia kwa wakati huo huo; naona umechelewa sana kuleta hapa

Haya mashirika ya ndege yapo covered nakumbuka mzigo ukipotea mikononi mwao yanaweza kulipa sina hakika vizuri ila nafikiri ni maximum ya 5M zaidi ya hapo unadai kwenye insurance yako kama unayo

hiki ndo na mimi nilikuwa najaribu kukieleza hapo juu
 
Last edited by a moderator:
MROSO wako gali Sana na jamaa aliyenisaidia hakuipeleka ofisini Kunisaidia kuepusha gharama Za kulipia ofisini akasema atafatilia yeye kama yeye, akawa amenipa moyo Sana Ata Sasa nimetoka kumpigia hapokei simu
 
Kwa bahati mbaya hapo utakuwa umekula hasara, kwa makubaliano ha kimataifa maximum unayostahili kulipwa kwa begi ni kama $1700, na mbaya zaidi hauna ushahidi kilichokuwepo kwenye hilo begi kwa hiyo hata hiyo itakuwa ngumu kuipata, na kama ni zaidi ya mwaka sasa maana yake chance za kulipata hilo begi sio nzuri kabisa.
 
mbere,

Pale Dubai wakati unakabidhi mzigo ilibidi wakupe "tag" au sticker ya mzigo ambayo unabaki na copy moja, nyingine inafungwa kwenye mzigo. Jee, ulipewa hiyo "tag"? Kama kwa sababu moja au nyingine hauna hiyo "tag", basi huna case. Vinginveyo, isingekuwa tatizo Swissport/shirika la ndege kuufuatilia huo mzigo. Binafsi naona umeibiwa JKNIA baada ya ndege kutua. Wa kuwafuata kwanza ni Swissport.
 
Ndugu yangu husikate tamaa maana haya mashirika ya ndege na insurance mbali mbali ndo huwa mchezo wao wanakusumbua ili utake tamaa uache ili wao wapate faida..

Ni moja wapo ya tricks zao na zinajuliana. Hivyo basi cha kufanya wakomalie tafuta risiti sehemu uliponunua mzingo (ingawaje sio lazima kuwa na risiti ila hapa napo watazungusha zungusha) na nenda nao tena ikibidi tafuta mwanasheria mwingine ambaya atakayeguswa na story yako ili awafungulie mashataka. Hapo watalipa tu hawana jinsi.

Muhimu sana husikate tamaa maana kukata kwako tamaa ndio faida yao na ndicho wanachokitaka.
 
Mara nyingi nikipanda ndege sipendi kuweka mizigo kwenye carrier nje. Ukipoteza mzigo ni vigumu sana kuupata. Pole
 
Kwa nini ulitumia usafiri wa Ethiopian Airline ambayo ina hub yake Addis Ababba badala ya kutumia Emirates Air au Fly Dubai? Just thinking aloud. Ukishanijibu nitapata mwanga wa kukushauri
 
Ni usafiri nafuu haswa Kwa mfanya biashara ndugu, kwa siku niliyosafiri nauli kwenda na kurudi kulikuwa na ofa haikufika laki 7, na nilizingatia maela yenyewe mengine ni mkono yafaa kubana matumizi
 
Na kila wakiulizwa wanasema upo ethiopia wanautafuta nilikata tamaa zaidi Kwasababu NILIKATA JAMAA MWANASHERIA WA KAMPUNI INAITWA MROSO IPO DAR NA ARUSHA, AKANIAMBIA KWAKUWA SINA HELA ATANISAIDIA ILA ATADAI 100ML PAMOJA NA USUMBUFU, WANDUGU KWELI, SIKUWA TENA NA KITU ADI LEO JAMAA HAPOKEI SIMU YANGU

Mroso lazima angedai HELA nyingi mjomba!

Ila kama Huna kipato cha kutosha, achana na hilo suala la Reputable law firm (kutafuta)

tumia njia nyingine tu, but njia rahisi ya kuipata hiyo mizigo yako ingekuwa ni kupitia kwa hawa wanasheria!!

Naamini ungekuwa na hela ya Kutosha Mroso angekusaidia kiurahisi kupata mizigo yako.

Ni reputable Adv.
 
Sad pole sana mkuu, ila ninaomba ufanye hivyi kama unakumbuka duka ulilonunua mzigo na tarehe kuna watu wengi sana wanaenda Dubai andika barua ya kuelezea story yako tuma copy ya passport maana vitabu vya receipt vinacopy waombe wakupe certified copy ya hiyo copy, kuna wakati rafiki yangu alinunua vitu nje hakujua kuwa kuna kurudishiwa hela bongo baada ya karibia mwaka huku bongo ndio akasikia na receipt alishatupa huko aliandika barua majuu na receipt nyingine ikaja. mbere
 
Last edited by a moderator:
Nimeguswa sana na story yako. usikate tamaa fuatilia vigezo mhimu ambavyo wataalamu wamekuambia stahili yako lazima ipatikane. hakuna aliye juu ya sheria na hata akitumia ngazi kuwa juu ya sheria moja nyingine itakuwa juu zaidi yake. pole mkuu.
 
shida yako tujue umepanda ndege tu huna lolote


kama unataka watu wasiingie kwenye shida mbn ujasema hyo shida yenyewe
 
Back
Top Bottom