Shirika la ndege la South Africa (SAA) liko hoi lakaribia kuwa mufilisi - Tanzania tuna jambo la kujifunza?

Black skin Sijui tuna shida gani kuhusu management.. ukikuta biashara kubwa ya wabongo weusi imesimama kwa Miaka 10..Ni Jambo la kumshukuru Mungu, Ukienda nje ya Nchi unapata wivu kuona a lots of family companies Zina historical ya Miaka 50 kuendelea, yaani mtoto anasoma na kuandaliwa kuongoza biashara za family. Black skin akifa Mtu na biashara zake zinamfuata..back to the topic kuhusu ATCL kwa Sasa tunyamaze kimya siku azigandi..2026..Akiwa chato anaitwa mstaafu ukweli utajulikana tu.
 
Hasara ya ATCL ni tayari huku bado tunanunua ndege hovyo hovyo kama vile tunanunua toy za kuchezea. Nawaambieni ni suala la muda tu, na hakuna jambo litakalofichwa kama hasara ya ATCL. Mashirika mengi sana makubwa ya ndege duniani yanaendeshwa kwa hasara, sisi hatufanyi utafiti kabla tunafanya mambo ya kujiletea sifa za kupuuzi kwa hasara ya walipa kodi.
 
Angalia kampuni za simu hapa nchi I zinazoendeshwa na mataifa mwingine halafu compare na TTCL huo ni mfano tu

Kwa kweli tunaitaji mataifa mengine kutusaidia uendeshaji wabongo wengi ni wapigaji
 
Mkuu una maanisha ma "air hostages"?
Ewaaa! Mara nyingine nafikiria maamuzi juu ya uendeshaji wa TTCL unafanywa na watu ambao hawajui hata hawa wahudumu wanaitwaje, tutafika? Busara ni kwamba usiingilie kabisa uendeshaji wa TTCL.
 
Kigoma hadi leo hatujaunganishwa kwa laki.. shame!!
 
Kigoma hadi leo hatujaunganishwa kwa laki.. shame!!
Halafu hivi kwa nini tumewapa Kenya Airways safari kibao za Dar-Nairobi kwa siku na sie hatuna hata moja kwa ajili ya ATCL? Kwa nini hauwapunguzii KQ ili tuchukue baadhi ya hizo safari?
 
Angalia kampuni za simu hapa nchi I zinazoendeshwa na mataifa mwingine halafu compare na TTCL huo ni mfano tu

Kwa kweli tunaitaji mataifa mengine kutusaidia uendeshaji wabongo wengi ni wapigaji
Ni kwa kuwa tunafanya mambo kwa kupenda sifa au kwa ajili ya umaarufu wa kisiasa! Unajua ujiko wa kisiasa unaotokana na sherehe ya kupokea Dreamliner tuliyonunua kwa pesa yetu wenyewe? Hayo mambo mengine ya kama tutaendesha shirika kwa faida au hasara hayachukui uzito. Tunaweza kuagiza Dreamliner sita kwa ajili ya ujiko tu, na kuzi park bila kazi baada ya sherehe ya kuzipokea, maana tunaagiza bila hata kuwa tumepanga zitakwenda wapi au kama tayari tuna mapailot wa kuziendesha! Tukishauriwa tunasema sipangiwi!
 
Mbona nimesikia sisi tunapata faida,hao jama itakuwa hawajui biashara ya ndege,watukodishe kama vipi tuongeze route mpaka Washington DC.
 
Mbona nimesikia sisi tunapata faida,hao jama itakuwa hawajui biashara ya ndege,watukodishe kama vipi tuongeze route mpaka Washington DC.
Mkuu, hivi unategemea unaweza kutangaziwa kwamba ATCL inapata hasara, hata kama ni kweli inapata hasara? Ili viongozi wa upinzani wapate jambo la kumzodoa Magufuli? Kwa hiyo usitilie maanani sana ukiambiwa ATCL inapata faida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…