DOKEZO Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetelekeza Abiria Mwanza, hadi sasa hawajui hatma yao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
450
Reaction score
3,368
Safari yangu ya kurejea Dar es salaam baada ya kukamilisha kazi yangu Bukoba imeanza asubuhi ya Februari 21, 2026 kwa ndege TC 101, mali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Kasheshe imeanzia uwanja wa Ndege wa Bukoba, hauna umeme.

Baada ya kuwekwa foleni kwa masaa 3, baadae ilibidi wahudumu waanze kukagua msafiri mmoja mmoja manually kwa kumwaga chini vitu vyote kwenge begi na vifungashio bila kujali umebeba nini. Aibu gani hii?

Jambo hili lilifanya ndege ikawie kwa zaidi ya saa 1. Karne hii uwanja wa ndege unakosa backup ya Jenereta? Tiketi zinaandikwa kwa mikono. Ni maajabu!

Baada ya kufika Mwanza mchana, ilibidi nichukue hotel nipumzike kidogo, na baadae saa 3:30 usiku kusogea airport ili niendelee na safari yangu ya DSM kwa TC 103 (Air Tanzania). Kumbuka, safari hii awali ilikuwa nisafiri saa 5:30 usiku, juzi nikapata email imepelekwa saa 7 usiku, lakini nilipokuwa hotelini nikaamua kupiga simu ATCL kuhakikisha, nikaambiwa imerudishwa saa 5:30 usiku. What a confusion!

Baada ya kufika airport saa 3:40 usiku, nilikuta mlango umefungwa, watu wamejaa, check in haijaanza. Nikajiongeza tu kuwa hapa safari hakuna.

Baadaye kama saa 4:10 hivi mlango ulifunguliwa, kufika ndani sehemu ya kupata tiketi mdada aliyekuwa anahusika akanipa taarifa kwamba safari imepelekwa tena saa 7 usiku. Nilichoka.

Ikabidi nisubiri hiyo saa 7. Ukimya ukatawala, na baada ya watu kuanza kuhoji ndipo wahusika wa uwanja wakatangaza Ndege haiji, nimeenda Kilimanjaro kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi, na hakutoa majibu ya itakuja lini na saa ngapi Mwanza. Fikiria, ndege imebadilishiwa muda wa safari mara 3, umefika airport umefanya check in, unasubiri muda wa safari, kisha unaambiwa haiji, na huna uwezo wa kutoka nje ya Airport.

ATCL, kwanini mnatesa abiria? Kuna wanawake wajawazito hapa, watoto wachanga, wazee, lakini hata sisi vijana hatupaswi kufanyiwa hivi.

Namaliza kwa wito, wakumbukeni abiria hawa. Pelekeni ndege Mwanza ibebe abiria wenu wanaoteseka kwa hela waliyolipia wao wenyewe. Acheni kufanya kama usafiri huu ni hisani. Wapatieni huduma inayostahili.

UPDATE: Saa 11:50 Asubuhi mlango emefunguliwa abiria waingie kwenye mabasi waelekee sehemu ya kupanda ndege. Mfumo wa ku scan tiketi umegoma, abiria wamenzisha vurugu, imebidi waruhusiwe kwenda kupanda bila ku scan.

Saa 12: 19 Asubuhi, Abiria wameanza kuingia kwenye ndege.

Saa 12: 45 Asubuhi: Safari imeanza.
 
Safari yangu ya kurejea Dar es salaam baada ya kukamilisha kazi yangu Bukoba imeanza asubuhi ya Februari 21, 2026 kwa ndege TC 101, mali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Kasheshe imeanzia uwanja wa Ndege wa Bukoba, hauna umeme.

Baada ya kuwekwa foleni kwa masaa 3, baadae ilibidi wahudumu waanze kukagua msafiri mmoja mmoja manually kwa kumwaga chini vitu vyote kwenge begi na vifungashio bila kujali umebeba nini. Aibu gani hii?

Jambo hili lilifanya ndege ikawie kwa zaidi ya saa 1. Karne hii uwanja wa ndege unakosa backup ya Jenereta? Tiketi zinaandikwa kwa mikono. Ni maajabu!

Baada ya kufika Mwanza mchana, ilibidi nichukue hotel nipumzike kidogo, na baadae saa 3:30 usiku kusogea airport ili niendelee na safari yangu ya DSM kwa TC 103 (Air Tanzania). Kumbuka, safari hii awali ilikuwa nisafiri saa 5:30 usiku, juzi nikapata email imepelekwa saa 7 usiku, lakini nilipokuwa hotelini nikaamua kupiga simu ATCL kuhakikisha, nikaambiwa imerudishwa saa 5:30 usiku. What a confusion!

Baada ya kufika airport saa 3:40 usiku, nilikuta mlango umefungwa, watu wamejaa, check in haijaanza. Nikajiongeza tu kuwa hapa safari hakuna.

Baadaye kama saa 4:10 hivi mlango ulifunguliwa, kufika ndani sehemu ya kupata tiketi mdada aliyekuwa anahusika akanipa taarifa kwamba safari imepelekwa tena saa 7 usiku. Nilichoka.

Ikabidi nisubiri hiyo saa 7. Ukimya ukatawala, na baada ya watu kuanza kuhoji ndipo wahusika wa uwanja wakatangaza Ndege haiji, nimeenda Kilimanjaro kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi, na hakutoa majibu ya itakuja lini na saa ngapi Mwanza. Fikiria, ndege imebadilishiwa muda wa safari mara 3, umefika airport umefanya check in, unasubiri muda wa safari, kisha unaambiwa haiji, na huna uwezo wa kutoka nje ya Airport.

ATCL, kwanini mnatesa abiria? Kuna wanawake wajawazito hapa, watoto wachanga, wazee, lakini hata sisi vijana hatupaswi kufanyiwa hivi.

Namaliza kwa wito, wakumbukeni abiria hawa. Pelekeni ndege Mwanza ibebe abiria wenu wanaoteseka kwa hela waliyolipia wao wenyewe. Acheni kufanya kama usafiri huu ni hisani. Wapatieni huduma inayostahili.
Hamkomi? Au mpaka siku liwabwage wote chini?
 
Ni kawaida yao, unafika destinantion alfajiri, kama ulifanya booking kwenye hotel flani ili ukifika upumzike kidogo, inabidi ukifika usilale kuhofia kupitiwa na usingizi ili usichengane na ratiba... yote hio kisa uzembe..
 
Hivi Mashirika ya Ndege wana kinga ya kutoshtakiwa kwa kupoteza Muda wa Watu?

Maana hii sio mara ya kwanza.
Kama ATCL ni mwanachama wa IATA lakini sidhani
Basi wanaweza kushtakiwa na abiria kama watakatisha nauli na kutelekeza abiria
Abiria atalipwa hela yake ya kulala hoteli ya angalau nyota 3 na gharama ya chakula hata Kama alilala Airport
 
Back
Top Bottom