DOKEZO Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetelekeza Abiria Mwanza, hadi sasa hawajui hatma yao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
CEO mnachaguana kama wajumbe wa Nyumba kumi. Uganda Airlines wamemtimua yule kuilaza wa kwao na sasa wamepata mu-Ethiopia mwenye experience ya airlines management . Hapo ATCL mtu wa marketing tu ni kichekesho
 
KWENYE FLIGHT RADAR status ya TC103 ni <unknown> kumbe mmepakiwa alfajiri hii poleni sana
 
Tatizo linaanzia kufanya kila kitu kwa mtizamo wa kisiasa, hiyo ndiyo chanzo cha mashirika yote ya umma kufanya vibaya. Hawatafutwi watu wenye uwezo wa kuyaongoza kwa mtizamo wa uwezo wa mhusika, bali watu wanateuliwa na kupewa nafasi hizo kama zawadi. Wanasiasa wanawateua watu wao kushika hizo nafasi kama hisani.

Mashirika kama Emirates, ukitizama kwenye management yao, kwa miaka mingi mkurugenzi mkuu siyo hata mwarabu, wanatafuta mtu mwenye weledi mkubwa bila ya kujali hata utaifa wake, mafungamano yake ya imani za kisiasa au dini, ndiyo maana wamefanikiwa. Kwetu kwanza anaangaliwa ana kadi gani ya chama cha siasa, ndani ya hicho chama alikuwa anamwunga mkono nani, n.k; anapewa nafasi kama shukrani au zawadi.

Utendaji duni wa mashirika yaliyo chini ya Serikali, hautakuja kukoma mpaka siku ambapo watendaji wakuu wa mashirika hayo watapatikana kupitia mifumo huru ya kupima weledi, na hawatawajibika kwa wanasiasa.
 
Haya ndo mambo ATC haitui Europe au North America ukiacha usalama pia delays/cancellations kama zote na hawawajibiki kwa lolote (sio accommodation wala meals kwa abiria).
Kwa namna hii ya uendeshaji ni vigumu sana kutua sehemu hizo.
Kama mtu ana appointment mda fulani tayari anakuwa tayari kashaikosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…