Mkuu ngoja nikuambie neno, ili usilete kuchongea watu bila sababu. NI kwamba katika sheria ya manunuzi ya serikali inasema kabisa magari gani yanapaswa kununuliwa, na huwa ni hizo Landcruiser na Pick up double cabin. Wakati fulani ilikuwa ni Land Rover Defender 110. Kwa hiyo hawa watu hawajiamulii, bali ni sheria inawapeleka kununua hayo magari. Bila hiyo sheria ungekuta wananunua Range Rover, Lexus, Jeep, BMW X5, Mercedes GLS nk.
Kuna wakati mradi wa EU hapa nchini walipata matatizo kwa kuwa wao walitaka kuagiza magari ya Ulaya, lakini sheria ikawa inawabana kununua magari ya Japan kulingana na sheria ya manunuzi ya Tanzania. EU wakaona kama wanalazimishwa kuwa promote Wajapan wakati fedha ni za Ulaya.
Kwa hiyo usimlaumu mtu wa serikalini au shirika la umma kununua hizo V8