Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

T TBC mmepoteza heshima mbele ya taifa mlichoifanyia chadema Leo ni kuihujumu hamkwenda pale kwa weledi.

Lengo lenu ilikuwa ni kuihujumu chadema na si kuitangaza mbaya zaidi mna hujuma za kitoto na za kishamba Sana.

Ujinga mlioufanya.

1.Aina za picha mlizochukua ni close lengo msionyeshe wingi wa watu.

2.Wakati mbowe anaongea mkakata sauti yake mkawa mnajadiliana utopolo wenu wa Bibi na bwana kwenye tv ya taifa Sasa swali!

Je lengo lilikuwa tuwasikie wale mtu na mkewe pale TBC au mbowe aliekuwa anaongea muda ule?

Mna mambo ya kishamba Sana TBC Ila ombeeni CCM ibaki madarakani mpaka mnaingia kaburini....!

Mbaya zaidi mnaofanya hujuma hizi ni vijana mnaotazamiwa kuishi muda mrefu mnatumika kishamba kuuwa weledi wenu wapumbavu kabisa nyie TBC.
 
Hivii nyie TBCCM mlishawahi kutangaza lile pingamizi la RAIS LISSU kwa huyo meko wenu?
 
TBC mnatufanya watanzania wajinga Sana mnatudharau Sana watanzania ila ombeeni Sana watanzania waendelee kulala usingizi unaochagizwa na wasanii na ujinga wa ndege kwaya na fly over ombeeni Sana TBC ujinga wa watanzania utamalaki mbwa nyie.
 
Mlivyowajinga mnadhani nasisi ni wajinga mlivyotegesha kamera zenu Leo tuliona ila kesho mtatumia mpaka drones halafu tutaona wakati anaongea mwenyekiti wenu je kutakuwa na mke na mume wanaongea muda huo huo? Kwenye studio zenu?
 
Mie mwenyewe nashangaa why hawajarushiwa mawe
CHADEMA ni wastaarabu sana utamaduni na utalaamu wa kuwatupia mawe viongozi wa upinzani wanaachiwa UVCCM kama walivyoonyesha kule Hai. TBC walifika kwenye uzinduzi wa Kampein ya CHADEMA ili kuwasaidia CCM kesho kwenye uzinduzi wao kujibu mapigo ndo maana kila viongozi walipoanza kuchambua CCM au Serikali sauti ilikatwa na kurudi Studio na kuwapa nafasi watangazaji kuunga mkono juhudi. CHADEMA wamefanya vizuri kuwafukuza waliletwa kupandikiza sumu kwa manufaa ya Magufuli na wataendelea kufanya hivyo mikutano yote wakiruhusiwa. Bloody dirty spies!
 
Maaskofu na mapadre wanasubiri kuiombea CCM kesho na sadaka jumapili.
 
TBC siku zote kimekuwa chombo cha habari njema za CCM, nadhani no vizuri mkafuata misingi ya vyombo vya habari vya habari vya umma! TBC iache kutumika na CCM na ibaki kuwa chombo cha umma!!!!
 
Pigwa wewe Risasi 16 kisha ukipona Ile ikawa kimya.
Taratibu tutaelewana tu
 
Wa kwanza kukatwa alikuwa Lema wa Arusha alipotaja tu jina la Magufuli kama ametaja Jina la Bwana Mungu wake bure, tumekatazwa na Amri Kumi za Mungu.
 
Alipo teuliwa yule Dr Lyooba nikawa na imani kuwa angekuwa ni muarobaini wa kuifanya tbc ijirekebishe lkn wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Naam, Ryoba Ayubu kabla ya kiteuliwa kuiongoza TBC alikuwa mtu wa kuaminiwa sana. Aliandika makala nyingi sana kwenye gazeti la Rai la kipindi kile, makala zenye kukemea linalofanywa shirika analo liongoza kwa sasa, alihimiza haki, alihimiza demokrasia,.............angalia anacho kifanya sasa hivi!. Inasikitisha sana.
 
Elizabeth Mramba acha upoyoyo na hao wazushi wenzako kina Mkama/Amini Anthony Mgeni , nimewajua kwasababu wote mlikuwa mlimani ,kwanini alivyoanza kupiga spana Lema mka mute sauti na kujiweka nyinyi na comment zenu? Uchambuzi unatakiwa ufanyika kipindi ambapo hakuna mtu anayetoa nondo labda kama MC anaongea.
 
Nimemsikiliza Mbowe akiwafukuza, kwa namna kuhamasisha umati sasa usishangae akiitwa polisi kutolea ufafanuzi lugha aliyotumia ambayo imetishia usalama wa wafanyakazi wa TBC.

Matatizo mengine CDM wanajitafutia
Si matatizoni ya kujitakia, bali uamuzi sahihi ulotakiwa kuchukuliwa. Hata kwa akili za chekechea utabaini kuwa TBC walikuwa pale kiunafki nafiki tu.
 
Ondoa !!
 
Tbc walijiminya wenyewe, walitoka ofisini kwao kwa ajili ya kurusha mkutano wa Chadema live, badala yake wakarusha mengine wanayo juwa wao. Kwa ufupi uwepo wao pale ulikuwa ni upotevu wa muda na matumizi mabaya ya nguvu kazi. Alowafukuza kawasaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…