Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Akili za CDM wote sawa kuanzia viongozi wao wa juu mpaka wafuasi wa mtaani.

Lazima watafute mtu wa kumtolea hasira zao mambo yanapoenda kombo, mkutano umeenda ndivyo sivyo kwenye umati awataki TBC warushe, ata JF ukimkosoa Lissu lazima kuna jitu litataka likutee hasira zake kwako.

Pamoja na kutaka kuona Magufuli anashinda lakini sio mapema hivi. Ikimbukwe asilimia kubwa ya kura millioni 6 za Lowassa 2015 zilipatikana Dar, kwa mapokezi ya Lissu mmh hapo kama vile hana chake.

Watu wengi wameshauri sana jamaa story yake ya risasi 16 ikishasikilizwa mara moja ndio imeshasikilizwa mara zote itachokwa mapema sana. Katoka huko yupo kuponda maendeleo na kazi ya Magufuli badala ya kusema atawafanyia nini.

CCM wanakazi nyepesi kweli, binafsi wala sishangai.
Sasa Kwanini hukuwashauri ccm wasifanye dhuluma, na ubakaji majimbo kwa kuwateka wapinzani, mapingamizi ya kijinga, polisi, takukuru nk, wakati CHADEMA wepesi tu?!!
 
We endelea kujiongopea hivi unafahamu bila ya hayo madaraja safari ya nusu 30 saa huku kijiji inaweza kuchukua masaa 3 kwa usafiri wetu; kama mtu an akimbizwa hospitali uwepo wa daraja linakuwa swala kufa na kupona. Halafu we unaona daraja halina tija, akili zenu zinawatosha wenyewe.
Acha porojo mkuu Yesu alifufua watu na bado akapigwa mawe sembuse huyu aliye jenga madaraja!
 
..Wawe pia Wawazi na Kueleza walichofanya hadi CHADEMA kufikia hatua ya kufanya walichowafanyia!
CHADEMA sio Wehu wa Kuanza kutimua Watu kwenye Mikutano!
TBC wekeni mambo hadharani...Mlifanya nini?
Mwisho wao ndiyo umefika wa kujipendekeza kwa ccm wakati wanalipwa kwa mishahara inayotokana na kodi za watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hili, Mbowe amekosea. Kama kiongozi wa chama ambacho kila wakati kinalalamikia serikali kwa 'kuminya' uhuru wa vyombo vya habari, Mbowe hakupaswa 'kuiminya' tbc kwa kuifukuza palepale mkutanoni bila hata kupata muda wa kutafakari athari za maamuzi yake. Ni mfano mbaya kwa chama kinachosema kipo tayari kushika dola na kutoa uongozi mbadala kwa nchi.
 
Mheshimiwa Daktari Ayoub Ryoba,
Mengi ya kufurahisha na ya karaha yamefanywsa na TBC tumeyapokea kabla ya uongozi wsako na sasa kipindi cha uongozi wako...
Lini TBC wakarusha mikutano ya upinzani hasa chadema? Wasubirie mikutano ya Nccr mageuzi na cuf ambayo ni matawi yao
 
Katika hili, Mbowe amekosea. Kama kiongozi wa chama ambacho kila wakati kinalalamikia serikali kwa 'kuminya' uhuru wa vyombo vya habari, Mbowe hakupaswa 'kuiminya' tbc kwa kuifukuza palepale mkutanoni bila hata kupata muda wa kutafakari athari za maamuzi yake. Ni mfano mbaya kwa chama kinachosema kipo tayari kushika dola na kutoa uongozi mbadala kwa nchi.
vibaraka wame fufurushwa uwanjani Nguvu ya umma imeshangilia sana
 
Back
Top Bottom