Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Pamoja na kwamba sihafikiani na maamuzi yakuwafukuzwa tbc yaliyoafikiwa na Cdm ila pia siwalaumu sana Cdm kwakuchukua hatua hiyo kwasababu kuna mambo yanakera tena ukizingatia yanafanywa na chombo cha Umma sasa yakiendelea kutazamwa tu tutajikuta tunakua na vyombo vya Umma mzigo visivyoweza kuleta mageuzi ya ustawi wa jamii.Lakini pia Tbc walipaswa wajue kua Cdm ni mshindani sawa na washindani wengine kama Act,Ccm na wengine na hichi ni kipindi cha kampeni kwahiyo walipaswa kujua lazima Cdm watakua na hoja zakuonyesha madhaifu ya mmoja wapo ya mshindani au serikali yenyewe.sasa kama wao wanajua hawawezi kusikia hoja za namna hiyo walipaswa kua na namna nyingine yakufanya tofauti na walichokua wanafanya.Ule ni utoto na kamwe hauwezi kulisaidia Taifa.Lakini pia niwakumbushe Wapinzani kua hichi sio kipindi chakulalamika au kufanya maamuzi kwa hisia na mihemko.
 
Tundu Lissu kweli kawashika MATAGA kunako.

TBC wanalia!
Polisi huko Twitter wanalia!

wameshikwa haswaaa!

View attachment 1551053
Kawashika sana na wana hofu nae sana
IMG_20200828_203405.jpeg
 
Mi sina chama lkn walichofanya CHADEMA ni upuuzi, walitakiwa kuwaacha waendelee na kazi yao. Kwa tendo lile ilikuwa ni hatari kwa usalama wa vyombo vyao na wakijua watangazaji pia. TCRA wana sheria na kanuni za maudhui, TBC hawataki kuingia mgogoro wa kulipishwa faini na TCRA.
We ni ccm
 
Chadema wamejiharibia. Hakutakuwa na chombo cho chote cha habari kitakachorusha wala kuandika kampeni zao. Watabakia twiter, instagram na yutube pekee ambako wateja wake hawazidi laki moja. Itabidi mgombea wao atembelee kila kijiji. Pesa ya kufanya hivyo hawana. Ile yakutoka kwa mabeberu itataifishwa.
 
Mwanasiasa yeyote makini awezi kukataa fursa ya bure ya kuwafikia wapiga kurawengi waliopo majumbani kwao.

Hizo ni hasira za mkizi...........

Hapo ni sawa na CDM kujinyima haki yao ya kusikilizwa na mamillioni ya wapiga kura kila watakapoenda huko mbeleni.

Uwezi laumu Azam na ITV wasipotokea kwenye mikutano yao ni kampuni binafsi; hila TBC wasipokuwepo na wewe unataka audience unaweza toa lawama.

Kupanga ndio kuchagua.
Wewe una kichaa!!
 
Mbowe alikosea pale ilikuwa wapewe dakika tano tu,kumi tano zilikuwa nyingi sana.
Hata hivyo iwe fundisho .....Kamanda wa anga alipaswa ndio apeperushe bendera kwa ujasiri ambao ameuonesha
hapa kuna neno la kuwauliza tbc ,hivi tangu chadema wanaanza mchakato wa kumpitisha mgombea wao lini wamerusha matangazo yao? pili leo wanazungumzia kwa mjibu wa kanuni za tume , why sio kwa mjibu wa sheria za tz kama chombo cha umma ? hata kama mie sijui sheria ila naamini zipo sheria ndongo zinazokiendesha chombo husika kama chombo cha umma , ukiacha tume .
mwisho ,
tbc kubali leo mlichemka na msiwalaum chadema maana mmesababisha leo watz kuingia gharama za kununua bando bila sababu , na kusema kuliopoti kwa ajili ya uslama wa vyombo halina tija maana hata leo mwenyekiti mbowe aliwapa notes na mkatekeleza na wala hakuna alie wagusa,
 
Nenda tu hapo Kibamba kawaulize kuna njia yao ya short cut ilikuwa aipiti bila ya daraja kufikia Mloganzila mvua zikinyesha ni kadaraja kadogo tu waulize sasa wenyeji uhuhimu wa hilo daraja kwao.

Hayo madaraja yanayounganisha wilaya na mikoa economic impact yake inabidi uandaliwe report, ndio ujue wewe ni mropokaji tu.
Kumbe ndo maana kuna vitu havifanyiki ili vije vitumike kama agenda kipindi cha uchaguzi.
 
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii.

TBC1 na TBC Taifa kama chaneli za umma zilikuwa zinarusha matangazo ya moja kwa moja kwenye uzinduzi huo kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Tume wa mwaka 2020, (kifungu e na j), kanuni za maadili ya tasnia ya habari; vyombo vya utangazaji vya umma pia vinao wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayorushwa hewani yanazingatia maadili ya taaluma na ya jamii.

Kitendo cha uongozi wa CHADEMA kutangaza kuwafukuza watangazaji wa TBC si cha kiungwana na kinahatarisha usalama wa watendaji hao na vifaa vyao.

Pamoja na kwamba TBC inapanga kutoa taarifa rasmi Polisi na kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sasa inasitisha rasmi kurusha matangazo ya CHADEMA hadi hapo watendaji wake watakapohakikishiwa usalama.

TBC inapenda kutimiza wajibu wake wa kisheria na imekuwa tayari, siku zote, kufanya kazi na vyama vyote vya siasa bila ubaguzi.

Hatuna shida na tbsccm
 
Wacha kiwagharimu lakini tuje tupate vyombo vya Umma vinavyojielewa.Huwezi kupiga hatua ya maendeleo kama nchi inakua na vyombo vyanamna ya Tbc.
Chadema wamekosa busara.walichafanya leo kuwafukuza tbc kitakuja kuwagharimu.
 
Hapo ni tatizo siwezi kubisha hii biashara ya wakurugenzi kunyima wapiga kura haki ya kuchagua kwakweli sio democracy.

Ningelikuwa mimi ndio Kiongozi upinzani sasa hivi nipo mahakamani naomba NEC isitishe zoezi la uchaguzi mpaka hilo jambo likae sawa, but thats just my thinking.
Basi ujue tu kwamba wakubwa zako ndani ya chama, wanajua ugumu wa huu uchaguzi, na wewe kudai kwamba CHADEMA ni wepesi sana, ni moja ya propaganda za kitoto! Propaganda hiyo inakusaidia wewe tu kuishi kwa matumaini, lakini haimshawishi Mtu yeyote!
 
Natarajia jukwaa la wahariri nao watatoa tamko. Kama walivyosimama pamoja pale Clouds media walipovamiwa pia watasimama TBC pia. Kwani vyote ni vyombo vya habari na maisha ya wana habari wenzao yametishiwa.
 
Mi sina chama lkn walichofanya CHADEMA ni upuuzi, walitakiwa kuwaacha waendelee na kazi yao. Kwa tendo lile ilikuwa ni hatari kwa usalama wa vyombo vyao na wakijua watangazaji pia. TCRA wana sheria na kanuni za maudhui, TBC hawataki kuingia mgogoro wa kulipishwa faini na TCRA.
Kukatakata matangazo haikua upuuzi?
 
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii.

TBC1 na TBC Taifa kama chaneli za umma zilikuwa zinarusha matangazo ya moja kwa moja kwenye uzinduzi huo kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Tume wa mwaka 2020, (kifungu e na j), kanuni za maadili ya tasnia ya habari; vyombo vya utangazaji vya umma pia vinao wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayorushwa hewani yanazingatia maadili ya taaluma na ya jamii.

Kitendo cha uongozi wa CHADEMA kutangaza kuwafukuza watangazaji wa TBC si cha kiungwana na kinahatarisha usalama wa watendaji hao na vifaa vyao.

Pamoja na kwamba TBC inapanga kutoa taarifa rasmi Polisi na kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sasa inasitisha rasmi kurusha matangazo ya CHADEMA hadi hapo watendaji wake watakapohakikishiwa usalama.

TBC inapenda kutimiza wajibu wake wa kisheria na imekuwa tayari, siku zote, kufanya kazi na vyama vyote vya siasa bila ubaguzi.

Hewa tbc waangalie walipo jikwaa wasiangalie walipoangukia iliugonjwa walionao uwatoke
 
Back
Top Bottom