gigabyte
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 5,717
- 6,465
Pamoja na kwamba sihafikiani na maamuzi yakuwafukuzwa tbc yaliyoafikiwa na Cdm ila pia siwalaumu sana Cdm kwakuchukua hatua hiyo kwasababu kuna mambo yanakera tena ukizingatia yanafanywa na chombo cha Umma sasa yakiendelea kutazamwa tu tutajikuta tunakua na vyombo vya Umma mzigo visivyoweza kuleta mageuzi ya ustawi wa jamii.Lakini pia Tbc walipaswa wajue kua Cdm ni mshindani sawa na washindani wengine kama Act,Ccm na wengine na hichi ni kipindi cha kampeni kwahiyo walipaswa kujua lazima Cdm watakua na hoja zakuonyesha madhaifu ya mmoja wapo ya mshindani au serikali yenyewe.sasa kama wao wanajua hawawezi kusikia hoja za namna hiyo walipaswa kua na namna nyingine yakufanya tofauti na walichokua wanafanya.Ule ni utoto na kamwe hauwezi kulisaidia Taifa.Lakini pia niwakumbushe Wapinzani kua hichi sio kipindi chakulalamika au kufanya maamuzi kwa hisia na mihemko.