Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Sasa Kwanini hukuwashauri ccm wasifanye dhuluma, na ubakaji majimbo kwa kuwateka wapinzani, mapingamizi ya kijinga, polisi, takukuru nk, wakati CHADEMA wepesi tu?!!
CCM bila Assistance ni hamna
 
Wangewachapa viboko kama ccm inavyoachiwa kuhubiri majukwaani kuwachapa viboko wapinzani.
 
Katika hili, Mbowe amekosea. Kama kiongozi wa chama ambacho kila wakati kinalalamikia serikali kwa 'kuminya' uhuru wa vyombo vya habari, Mbowe hakupaswa 'kuiminya' tbc kwa kuifukuza palepale mkutanoni bila hata kupata muda wa kutafakari athari za maamuzi yake. Ni mfano mbaya kwa chama kinachosema kipo tayari kushika dola na kutoa uongozi mbadala kwa nchi.
Ila kutesa upinzani ni vizuri?
 


Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii.

TBC1 na TBC Taifa kama chaneli za umma zilikuwa zinarusha matangazo ya moja kwa moja kwenye uzinduzi huo kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Tume wa mwaka 2020, (kifungu e na j), kanuni za maadili ya tasnia ya habari; vyombo vya utangazaji vya umma pia vinao wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayorushwa hewani yanazingatia maadili ya taaluma na ya jamii.

Kitendo cha uongozi wa CHADEMA kutangaza kuwafukuza watangazaji wa TBC si cha kiungwana na kinahatarisha usalama wa watendaji hao na vifaa vyao.

Pamoja na kwamba TBC inapanga kutoa taarifa rasmi Polisi na kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sasa inasitisha rasmi kurusha matangazo ya CHADEMA hadi hapo watendaji wake watakapohakikishiwa usalama.

TBC inapenda kutimiza wajibu wake wa kisheria na imekuwa tayari, siku zote, kufanya kazi na vyama vyote vya siasa bila ubaguzi.

Tulikuwa tunalisubiri tamko la TBC kwa hamu kubwa.Tumeskitishwa na kitendo cha CHADEMA na tunakilaani kwa nguvu zote.Huku mtaani tulishaanza kukaa roho juu maana yake hatukujua ule umma kwa amri ya viongozi wao baada ya hizo dakika kumi wangewafanya nini.Wafanyakaazi wa TBC tunawapa pole.Hiki ni chombo chetu cha umma tukiheshimu.
 
Sasa ndio uwazalizishe hivyo! [emoji50]
Uwazalizishe!!?? Nadhani ulikua na maana uwadhalilishe. Nani kawadhalilisha?? Hizi shule za siku hizi ni shida, kiswahili nacho kinawapa shida. God forbid.
 
Hii inaitwa SASA BAAASI

Toa wembe ni toe kisu kudadeki
Tumechokaaa
Mngekuwa na morali hii ya kutaka mabadiliko kwenye mfumo wa elimu ingekuwa ni uzalendo uliotukuka.
 
Mi sina chama lkn walichofanya CHADEMA ni upuuzi, walitakiwa kuwaacha waendelee na kazi yao. Kwa tendo lile ilikuwa ni hatari kwa usalama wa vyombo vyao na wakijua watangazaji pia. TCRA wana sheria na kanuni za maudhui, TBC hawataki kuingia mgogoro wa kulipishwa faini na TCRA.
Huna chama kipi? Na hata hufanani kuwa na chama.
 
Uwazalizishe!!?? Nadhani ulikua na maana uwadhalilishe. Nani kawadhalilisha?? Hizi shule za siku hizi ni shida, kiswahili nacho kinawapa shida. God forbid.
Achana na common mistake. Chukua muktadha! [emoji57]
 
Katika hili, Mbowe amekosea. Kama kiongozi wa chama ambacho kila wakati kinalalamikia serikali kwa 'kuminya' uhuru wa vyombo vya habari, Mbowe hakupaswa 'kuiminya' tbc kwa kuifukuza palepale mkutanoni bila hata kupata muda wa kutafakari athari za maamuzi yake. Ni mfano mbaya kwa chama kinachosema kipo tayari kushika dola na kutoa uongozi mbadala kwa nchi.
Umeifahamu vizuri TBC na kiifuatilia vizur mkuu? Watu hawaihitaji hata kama inaendeshwa kwa kodi zao. Tuiache ionyeshe vitu inavyopenda yenyewe kwa gharama ya jasho letu watanzania.
 
CCM (TBC) ilikwenda kufanya nini kwenye shughuli ya kitaifa...?

Wazee wa kuvizia kuteka na watu watu...miaka 5 wamezuia watu wasiongee leo eti wema sana...pambaf....komesha hao Yeboyebo!! aka Utoporo fc!!
Yeboyebo na Utopolo ni majina ya utani ya timu yangu Young African aka Yanga. Ingawa ni majina ya utani, ila si jambo jema kuinasibisha timu ya wananchi na hao wendawazimu wa sisiem, waliojaa dhulma. Ingekuwa vyema kuomba radhi kwa hilo.
 
Back
Top Bottom