Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Ile siku ilipotolewa taarifa kuwa vyombo vya habari vitaripoti kwa usawa mikutano ya kampeni ya vyama vyote mimi nilisisimka sana mwili nilipowawaza Tbc!nikajiuliza hili litawezekana kweli?
Sssa hata mwezi bado kupita tokea yatoke maamuzi yale yametokea haya!
 
To be honest, leo ukiiniuliza kama kuna mtangazaji yeyote wa TBC ninayemfahamu japo kwa kumuona kwenye TV, sidhani kama nitakuwa na jibu sahihi!

Let me guess... mtu pekee ambae nimemshika sura (sio jina) ni yule jamaa anatangaza mambo ya kale... sijui Zamadamu kufanya nini sijui!!!

Hivi kuna mwingine?! Ngoja nijaribu kufikiria zaidi... RIP Marin Hassan manake ndie pekee niliyekuwa nakufahamu kwa jina na sura!!

My point is: Nina miaka kadhaa sijawahi kabisa kusikiliza/kutazama the so called TBC lakini hapa JF huwa nasikia sikia kwamba, kabla ya hili suala la kampeni, TBC walikuwa hawatoi coverage kwa vyama vya upinzani!!

Kama ni kweli, basi namuunga mkono Mbowe kwa 101%! Huwezi miaka yote hii hutoi coverage kwa upinzani halafu kwenye kampeni wajifanye kutaka kutangaza live... Fvck y'all!!

Yaani leo wajifanye kutangaza kampeni za wapinzani ili wadanganye watu kwamba "kama chombo cha taifa, wametoa haki sawa kwa vyama vyote"?! Again, fvck y'all!!

Ni matumaini yangu ACT nao hawatakubali kutumika na hawa mbuzi, manake wanachotaka kufanya TBC hakina nia yoyote ya kweli zaidi ya kutaka kuwatumia wapinzani ili waonekane wametoa coverage kwa wote!!!
 
Watu wa ajabu sana. Lisu amezunguka mikoa zaidi ya 16 kupata wadhamini, TBC haikuona haja ya kurusha LIVE matukio, leo katika mazingira ya kusuasua imefukuzwa, watu wanahangaika. Watu wanaangalia wanachokipenda.
Hili ni fundisho kwa wanafiki woote kuwa haya ndiyo malipo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam, Ryoba Ayubu kabla ya kiteuliwa kuiongoza TBC alikuwa mtu wa kuaminiwa sana. Aliandika makala nyingi sana kwenye gazeti la Rai la kipindi kile, makala zenye kukemea linalofanywa shirika analo liongoza kwa sasa, alihimiza haki, alihimiza demokrasia,.............angalia anacho kifanya sasa hivi!. Inasikitisha sana.
Naanza kuamini kuwa ukisha kuwa ndani ya ccm wewe basi hata fikra zako zinapakwa rangi ya mboga mboga tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwasasa hakuna mtangazaji wa TiBC anaweza akaachishwa/akaacha kazi na kupokelewa kituo binafsi nchini au vile vya kimataifa, hakuna.
Na hii itawapelekea waishi kama misukule pale TiBC.
Mnawaona wanatabasamu kwenye camera lakini wanamadeni hadi kwa mangi hao
 
Ficha upumbavu wako na ionyeshe hekima yako.....

Mifumo yote ya kishenzi ikiwemo elimu inayosimamiwa na fisiemu itabadilika kwa kuwaondoa ccm kwa sanduku la kura na si vinginevyo

Ila kwasababu kuna masikini wa akili wengi kama wewe bado mnaunga juhudi za ccm yenye mfumo huo mbovu unaousemea wa elimu acha tuendelee kuisoma namba

Wenye akili ya ziada hawaoni kama kuitoa ccm madarakani ndio solution kwenye kivuli cha kuaminishwa kuwa ni demokrasia.

wenye akili ya ziada wanajua kutenga ukweli na siasa.

mabadiliko ya kweli yanaanza na wewe (self-government) kamwe usitegemee mtu fulani aje akuletee mabadiliko uanayotaka huo ni utahira.

CDM wamenisikisha sana kwa kuwa na ujasiri wa hata kuvunja amani ya taifa la mama zao kwa kivuli cha eti demokrasia uchwara kwa kutegemea backup ya wadau fulani wakidhani watapata wanachotaka huo ni utahira uliopindukia.

iko wapi Libya ya gadafi na Libya ya demokrasia ya wazungu walioitaka kwa kumuondoa mzalendo 🙁
 
Walikuwa wanakatisha katisha matangazo.

Ni yale yale yule marehemu alipigwa kule jangwani.

Wamshukuru mbowe kuwatimua maana watu wangewaadhibu vibaya.
 
Mlivyokuwa mnazima sauti na kuanza kuongea porojo zenu pindi wazunguzaji wanapoanza kushusha nondo mlidhani wananchi hawaoni? Ingekuwa mkutano wa ccm mngefanya hivyo?

Kanuni za uandishi wa habari unazijua?
 
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii.

TBC1 na TBC Taifa kama chaneli za umma zilikuwa zinarusha matangazo ya moja kwa moja kwenye uzinduzi huo kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Tume wa mwaka 2020, (kifungu e na j), kanuni za maadili ya tasnia ya habari; vyombo vya utangazaji vya umma pia vinao wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayorushwa hewani yanazingatia maadili ya taaluma na ya jamii.

Kitendo cha uongozi wa CHADEMA kutangaza kuwafukuza watangazaji wa TBC si cha kiungwana na kinahatarisha usalama wa watendaji hao na vifaa vyao.

Pamoja na kwamba TBC inapanga kutoa taarifa rasmi Polisi na kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sasa inasitisha rasmi kurusha matangazo ya CHADEMA hadi hapo watendaji wake watakapohakikishiwa usalama.

TBC inapenda kutimiza wajibu wake wa kisheria na imekuwa tayari, siku zote, kufanya kazi na vyama vyote vya siasa bila ubaguzi.
News Alert: - Yaliyojiri kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu katika viwanja vya Zakheim Mbagala, TBC Wafukuzwa

Uhuni wa kukata sauti ni ungwana....kweli nyani haoni kundule
 
Mtumishi wa Mungu anaejielewa duniani ni sheik ponda Isah ponda basi
 
Kifupi tu ni kuwa mmerahisisha sana kazi ya kutowapa airtime wapinzani, sasa mtakuwa hamna sehemu ya kulalamika kwamba hamtangaziw
 
Tbc walienda kufanya nn?
Wao wanajua fika matamshi ya chadema ni sumu kwenye mic zao Sasa wao walienda kufanya kitu gani?

Ni kwasababu walijua watakaribishwa na kuruhusiwa kufanya wapendavyo; pamoja na kukata matanga, nondo zinaposhushwa. Kwa bahati mbaya kwao. Tumeshachoshwa na unafiki wao!
 
TBC hawakupaswa kuondoka ktk eneo hilo, wameonyesha unyonge sana! jeshi la polisi lilikuwepo ambalo lipo pale kulinda watu wote na mali zao kwa nn waliondoka kutii amri ya mbowe?!huu ni udhaifu!! hawakupaswa kuondoka maana walikuwa pale kuripoti, na ifahamike kuwa tbc ni chombo cha wananchi wote,
ombi langu kwa uongozi, pangeni safu yenu vizuri ktk kipindi hiki cha kampeni, wekeni watu makini na imara ktk mchakamchaka huu, ondoeni watu walegevu na wasio jiamini........sio unaambiwa toka basi unaondoka kama vile mwizi au kibaka !!
lkn pia kauli ya mbowe kuwa fukuza waandishi kama wezi ambao walikuwa kazini ni kitendo cha uchochezi
 
Back
Top Bottom