Shirika linaweza kutoa gawio (dividends) hata kama limepata hasara

Shirika linaweza kutoa gawio (dividends) hata kama limepata hasara

kwema wanajf,
kumekuwa na watu wanasema ATCL ilipata hasara kwa hiyo haikupaswa kutoa gawio dhana ambayo sio kweli kwa kuwa gawio hutoka kwenye cash flow iliyopo kwenye shirika na sio mpaka pawe na faida kwenye financial statement. kama cash flow ipo gawio linatolewa vizuri tu. Tena hata kama shirika limepata hasara hukopa kulipa gawio japo hio njia ni so risk. Nashangaa hata CAG Uttoh hajui gawio hupatikana vipi nabaki nasema hiiiiiiii
Asante kwa uzi huu soma hapa
Na Zitto Kabwe

Kwamba Mashirika ya umma nchini yanamkabidhi Rais cheki za magawio (dividends) ya faida zao ni ama Ofisi ya Rais inafanya Siasa au hawajui maana ya gawio.

Tukiwa Bunge la 9, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC na baadaye PAC) ililishauri Bunge kufanya marekebisho ya Sheria ya baadhi ya mashirika ya umma Ili kiwango fulani cha Mapato ghafi (turnover) kitolewe Serikalini kama maduhuli ya Serikali.

Serikali ya wakati huo ilikubali na Sheria zikabadilishwa na kutenga 15% ya Mapato ghafi ya Taasisi za Umma kuwa Mapato ya Serikali kuingia Mfuko Mkuu wa Hazina. SIO FAIDA maana mashirika haya mengi hayana faida. Faida ya TCRA ni nini? Ama EWURA? Ama TANROADS?

Kusema Rais anakabidhiwa gawio la faida ya mashirika ya umma ni ulaghai ambao hauna maana yeyote, kwani Taarifa za Ukaguzi za Mashirika hayo zitaonyesha kuwa hakuna faida (na hivyo hakuna gawio), na hivyo kuumbuka kwa Serikali yenyewe.

Kinachotolewa ni nini? Haya ni maduhuli tu, ama ni kodi maalumu ambayo imewekwa kwa mashirika kwa kiwango cha 15% ya Mapato ghafi. Maduhuli au kodi hii imekuwa ikilipwa miaka yote ya nyuma. Sielewi ni kwanini sasa Rais amewaleta mbele wakuu wa mashirika Eti kutoa gawio! Gharama za kuwaleta hao wakuu wa hizi taasisi hazikupaswa kuingiwa kabisa, kwani kodi hizo hukatwa moja kwa moja kuingia Mfuko Mkuu wa Serikali. Sielewi hizi hadaa ni za Nini?

Ni muhimu pia kueleza kuwa kuna hoja ya Ukaguzi ya CAG kuhusu makato haya kwa baadhi ya taasisi. Kwamba makato haya yanapaswa kuwa ‘Tax deductibles’ - yaani wakati wa kukokotoa kodi ya Mapato ya baadhi ya Mashirika malipo haya yanapaswa kuondolewa kwanza.

Hata hivyo TRA wamekuwa hawafanyi hivi na hivyo kukuta mashirika kama TANAPA, NCAA, TPA nk yanalipa Fedha zaidi ya yanavyopaswa kulipa na kusababisha shughuli zao za msingi kushindwa kutekelezwa.

Watanzania msihadaiwe leo, hatupokei gawio, bali tunapokea maduhuli tu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 23, 2018.
Ni maduhuli na sio dividends.
P
 
dividend is a distribution of profits by a corporation to its shareholders.[1] When a corporation earns a profit or surplus, it is able to pay a proportion of the profit as a dividend to shareholders. Any amount not distributed is taken to be re-invested in the business (called retained earnings). The current year profit as well as the retained earnings of previous years are available for distribution; a corporation is usually prohibited from paying a dividend out of its capital. Distribution to shareholders may be in cash (usually a deposit into a bank account) or, if the corporation has a dividend reinvestment plan, the amount can be paid by the issue of further shares or by share repurchase. In some cases, the distribution may be of assets.
Sijui nikupe heko au hongera, yaani mtu ukizoea ujinga unakuwa mjinga hata kwa vitu visivyohitaji ujinga.
 
Umeona kipi kinachosapoti story yako ya uongo? Hapo waliposema assets zinaweza kutumika kama dividend unajua ni katika situation gani? Je, hiyo situation ATCL waliifikia na ni assets zipi zilikuwa distributed kwa Wabia?
A company’s dividends should be coming out of its cash flow, which can still be positive even if the company makes a loss. The company may make a loss for a variety of reasons, such as depreciation of assets, or it may have made some other investments of its own that have not yet paid off and so forth, so a loss does not intrinsically mean the company is in trouble. As such, some companies can make a loss and keep paying dividends without any concern.
 
Umeona kipi kinachosapoti story yako ya uongo? Hapo waliposema assets zinaweza kutumika kama dividend unajua ni katika situation gani? Je, hiyo situation ATCL waliifikia na ni assets zipi zilikuwa distributed kwa Wabia?
situation inajulikana lakini kampuni kurekodi loss kwenye p&l inaweza kuwa na positive cashflow ikalipa gawio au kama kuna earning fom previous years au pia kama inaweza kopa itafanya hivyo inategemea na situation
 
Siyo kweli.

Mimi ni mwanahisa wa Crdb dividends tunapewa benk inapopata faida.

Kwanza wanalipwa preffered shareholders halafu ndio sisi makabwela yaani ordinary!
inategemea na situation wakati mwingine haiko hivyo
 
Back
Top Bottom