Shiriki Katika Kudumisha Ubora na Usalama wa JamiiForums, tumia REPORT button

Waambie wakubwa watufungulie Jf au kama hutaki tuanze na majaribio ya kureport hii post maana tumechoka ma VPN
 
Max weka jukwaa la malalamiko na lia lia FC 😹😹😹

Wengine wanaanzaga shengesha wenyewe. Yakiwazidia wanaanza kujiliza huko HQ..

Mimi adui nnayemmudu siwaachii mods ni bampa to bampa..!!
 
Ndugu Maxence Melo kuna wale wanaotukana matusi ya nguoni na kutoa lugha za kuudhi wanaposhindwa hoja katika kutetea vyama vyao vya siasa.

Naomba muwashughulikie ipasavyo memba hao kwa maslahi mapana ya jukwaa hili pendwa.
Asante
 
Max weka jukwaa la malalamiko na lia lia FC 😹😹😹
Wengine wanaanzaga shengesha wenyewe. Yakiwazidia wanaanza kujiliza huko HQ.. Mimi adui nnayemmudu siwaachii mods ni bampa to bampa..!!
Kabisa km mie, ni kwenda nao sambamba.
😂😂😂😂
 
Umesomeka mkuu....mie nitatumia TAFSIDA....hapa ndio mahala pangu pakee pa kutolea SUMU...🙂🙂🙂
 
Siku hizi kuna wanachama ambao hutoa matusi haraka sana bila kutambua kuwa matusi hayo ni open book.

Badala ya kujadili mada kwa hoja wau hutumia matusi zaidi.

Hata wakongwe kama mimi ninapokuta natukanwa na kijana anayeweza kuwa mjukuu wangu nikamsihi kuwa awe mstaarabu lakini akazidi matusi basi huwa namwonyesha kuwa nilianza kutukanwa kabla hajazaliwa hivyo nina akiba kubwa sana ya matusi pia.
 
LHata wakongwe kama mimi ninapokuta natukanwa na kijana anayeweza kuwa mjukuu wangu nikamsihi kuwa awe mstaarabu lakini akazidi matusi basi huwa namwonyesha kuwa nilianza kutukanwa kabla hajazaliwa hivyo nina akiba kubwa sana ya matusi pia.
Nimecheka sana.

Ndo maana tumeweka hizi tools.

Usijichoshe mkuu wangu; tena kwa status yako - post ukii-report mara moja tu, instantly inaondoka online hadi iwe reviewed.

Pole, ila umenichekesha sana
 
Ndugu Maxence Melo kuna wale wanaotukana matusi ya nguoni na kutoa lugha za kuudhi wanaposhindwa hoja katika kutetea vyama vyao vya siasa.

Naomba muwashughulikie ipasavyo memba hao kwa maslahi mapana ya jukwaa hili pendwa.
Asante
Anza kwa kuwashughulikia kwa kusaidia kuondoa posts zao wewe.

Do not entertain them, report na immediately posts zao zitapotea na wengine hawataona matusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…