Shirikisho la mpira Africa (CAF) limeizawadia Simba sc tuzo ya Mashabiki Bora katika michuano ya African football league

AFRIKA KUSINI: SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewazawadia mashabiki wa timu ya Simba tuzo ya mashabiki bora wa michuano ya AFL.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Muhene 'Try Again' nchini Afrika Kusini kushudia fainali ya AFL.

Baada ya kupokea tuzo hiyo kiongozi huyo ametuma salamu za pongezi kwa wanasimba.

"Tuzo hii ni kwa kila shabiki wa Simba. Kuja kwenu uwanjani kushangilia timu yenu kumeiwezesha timu yetu kushinda Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL. Pongezi nyingi kwenu." Amesema kiongozi huyo.

MAONI YANGU: Mashabiki hawajaiangusha timu Bali timu inawaangusha mashabiki.

======

Mashindano ya AFL yalianza 20,10,2023 ikiwa ni mashindano mapya kabisa yaliyohusisha timu 8, ambapo Simba sports club ya Tanzania, ilipewa fursa ya kuwa mwenyeji wa sherehe ya ufunguzi wa michuano hiyo na kupigwa mechi ya ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly, ambapo kwa mechi mbili walitoka suluhu ya 2-2( Soma zaidi)na 1-1(Soma zaidi )na goli la ugenini kuwaondoa Simba kwa hatua ya awali ya robo fainali.

Mashindano hayo kwa msimu huu yamefikia tamati leo 12, 11,2023 kwa kuzikutanisha timu 2 zilizofanikiwa kufika fainali za Widad casablanka na Mamelodi Sandawons ambapo Mamelod ameibuka mshindi na kubeba ubungwa kwa mara ya kwanza. (Soma zaidi)

Katika tuzo zilitolewa na Simba imepata tuzo ya mashabiki bora baada ya kujitokeza kwa wingi siku ya ufunguzi wa AFL kweye uwaja wa Benjamii Mkapa.

Kombe la nidhamu, kombe la ushabiki. Hizi huwa ni tuzo kwa timu zilizofeli, fuatilia kuanzia Shule mtaniambia.
 
Tofautisha tuzo ya nidhamu kwenye mashindano ya gongouto na hizi tuzo unazopewa mbele ya viongozi na macho ya Africa yanatazama. katika ulimwengu wa soka hii ni nzuri kwenye ligi yetu hata ukitaka kusajili mchezaji mwenye ushindani unakuwa na kanafasi, mchezaji anajua naenda kwenye ligi ambayo kuna vibe na hakujapoa.
 
Baada ya kuwaingizia mabilion ndio wanakuja kuwaliwaza na tuzo za kipumbavu kiasi hiki?.
 
Mnapo msakama.mangungu mnakosea.wakuwasakama.ndio hao akina JARIBU TENA
 
AFRIKA KUSINI: SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewazawadia mashabiki wa timu ya Simba tuzo ya mashabiki bora wa michuano ya AFL.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Muhene 'Try Again' nchini Afrika Kusini kushudia fainali ya AFL.

Baada ya kupokea tuzo hiyo kiongozi huyo ametuma salamu za pongezi kwa wanasimba.

"Tuzo hii ni kwa kila shabiki wa Simba. Kuja kwenu uwanjani kushangilia timu yenu kumeiwezesha timu yetu kushinda Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL. Pongezi nyingi kwenu." Amesema kiongozi huyo.

MAONI YANGU: Mashabiki hawajaiangusha timu Bali timu inawaangusha mashabiki.

======

Mashindano ya AFL yalianza 20,10,2023 ikiwa ni mashindano mapya kabisa yaliyohusisha timu 8, ambapo Simba sports club ya Tanzania, ilipewa fursa ya kuwa mwenyeji wa sherehe ya ufunguzi wa michuano hiyo na kupigwa mechi ya ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly, ambapo kwa mechi mbili walitoka suluhu ya 2-2( Soma zaidi)na 1-1(Soma zaidi )na goli la ugenini kuwaondoa Simba kwa hatua ya awali ya robo fainali.

Mashindano hayo kwa msimu huu yamefikia tamati leo 12, 11,2023 kwa kuzikutanisha timu 2 zilizofanikiwa kufika fainali za Widad casablanka na Mamelodi Sandawons ambapo Mamelod ameibuka mshindi na kubeba ubungwa kwa mara ya kwanza. (Soma zaidi)

Katika tuzo zilitolewa na Simba imepata tuzo ya mashabiki bora baada ya kujitokeza kwa wingi siku ya ufunguzi wa AFL kweye uwaja wa Benjamii Mkapa.

Onyesha katika picha wapi imeandikwa Simba Fans!

Try Again ametuwakilisha Watanzania wote kupokea hiyo tuzo na inatakiwa ipelekwa TFF!
 
Back
Top Bottom