Habari,
Hili shirikisho letu la mpira Africa limekaa kizamani sana kwa kuendelea kutukuza na kukumbatia kanuni zisizo na faida Wala manufaa kwa mpira wetu.
Hili la fainali kuchezwa nyumbani na ugenini ni jambo la hovyo lisilokua na faida chanya kwa mpira wetu.
Sioni mantiki ya kanuni hii ya kuchezwa kwa fainali nyumbani na ugenini zaidi ya kuona kuzipa timu flani za mataifa ya kiarabu kutumia mbinu chafu katika kutafuta ushindi kwa wapinzani wao.
Swala jingine ni hili la goli la ugenini nalo naona kama ni upuuzi tu kwa mpira wetu hizi ni kanuni zilizopitwa na wakati na hazifai kwa mpira wa kisasa.
Ushauri wangu kwa CAF waondoe hizi kanuni mbili za fainali kuchezwa nyumbani na ugenini na hii ya goli la ugenini,Badala yake fainali iwe moja na ichezwe kwenye uwanja ambao ni mgeni kwa timu zote mbili. Na hili la goli la ugenini lisiwepo badala yake fainali ichezwe kwa dakika tisini kama hakuna matokeo ziongezwe dakika thelathini na endapo kutakua hakuna matokea pia basi mchezo uamuliwe kwa mikwaju ya penati.