Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa Orodha mpya ya Vilabu Bora Afrika kuelekea msimu mpya 2024/25

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa Orodha mpya ya Vilabu Bora Afrika kuelekea msimu mpya 2024/25

Simba ving'ang'anizi. Tujitahidi tufike nusu fainali,la sivyo tutashuka
Mwaka huu target ni kubeba ndoo kabisa ama sivyo hawa vyura watatuzidi na walivyo na kelele patakuwa hapakaliki. Point za CAFCC ni ndogo kuliko za CAFCL.

Zamalek ilishajifia kitambo, huu mfumo wa kufanya ranking kutokana na points ni WA kijinga sana, zamalek anakaa hapo kutakana na mafanikio ya miaka 10 iliyopita

Wafanye wawe wanafanya ranking hata ya misimu mitano nyuma
Zamalek wamesharudi
 
Mabingwa wa kombe la shirikisho barani afrika msimu uliopita unasemaje kua wamejifia unalijua soka kweli wewe?

Kama utopolo kufika fainali ya kombe la shirikisho walifanya sherehe na ikawabust kupanda kwenye rank za CAF wewe ni nani uwadharau mabingwa au haujui kia Zamalek ndo mabingwa wa kombe la shirikisho?
Zamalek ameshajifia, ni sawa na Al ahly kuja kushangilia kuchukua shirikisho, au man u wanavyofurahia kuchukua Europa/fa
 
Ni suala la muda tu WANANCHI kuingia top 10, subiri CAFCL ya msimu huu iishe
 
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa Orodha mpya ya Vilabu Bora Afrika kuelekea msimu mpya 2024/25
.
1. Al Ahly (Egypt) – 87 points
2. Esperance (Tunisia) – 61 points
3. Wydad AC (Morocco) – 60 points
4. Mamelodi Sundowns (South Africa) – 54 points
5. Zamalek (Egypt) – 48 points
6. RS Berkane (Morocco) – 42 points
7. Simba (Tanzania) – 39 points
8. Petro de Luanda (Angola) – 39 points
9. TP Mazembe (DR Congo) – 38 points
10. CR Belouizdad (Algeria) – 36 points
.
Chama lako namba ngapi hapo __!![emoji116]

Utopolo ni kama wanafanya harakati za Pimbi

View attachment 3069484
Sisi kama Uto....hatukubali hili
 
Kwenye hiyo top 10 kwa sasa hakuna timu ya kuifunga Yanga, kama unabisha angalia timu mbili hapo ndani ya msimu mmoja zimefungwa 5 na YANGA na nyingine 4
 
Simba tuwe makini sana, points zetu zimefanana na timu nyingine, na kusogelewa sana na walio chini yetu.
 
Yanga hatuna nongwa. Tukikutana na yoyote tunampimia tu.. bao 4 au 5 ikipendezwa atakula mpaka 8 kutegemea tu kakaa style gani chuma mboga au popo Kanyea mbingu. Akawasimulie wenzie huko URENKINI
 
Sasa mbona list nzima hamna timu ya kuifunga yanga aisee Africa kweli ni utapeli yaani mizigo ndio klabu Bora 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom