Shiza Ramadhani Kichuya, moto unaozimika taratibu

Ayenda M

Member
Joined
Jan 4, 2018
Posts
98
Reaction score
132
Katika ulimwengu wa burudani hususani katika soka kuna wachezaji watoa burudani na wachezaji wa mpira. Pia kuna wale wanaokupatia vyote viwili kwa wakati mmoja.

Pia katika soka kuna wale wachezaji hupenda kutumia mguu wa kushoto. Kule ulaya kuna wachezaji tunawahusudu kama Messi, Alba, Ozil, Alaba na wengineo wengi. Vipi hapa bongoland, nani asiyemjua Shiza Kichuya, Zimbwe Jr., Miquisson na wengineo wengi. Hawa watu wapo very talented!

Raha ya wachezaji wa namna hii ni kuwa akiwa anaujua mpira, anakuonesha kuwa kweli mpira ni kazi yake.

Pale Simba kuna Shiza Ramadhan Kichuya, Mluguru fulani hivi mwenye kimo cha kupanda minazi. Guu lake la kushoto limetengenezwa kwa ajili ya kuwaadhibu mabeki, kuwatesa viungo na kuwamaliza makipa. Yanga wanamkumbuka vizuri mwaka 2017 mchezo wa round ya pili na goli lake la nje ya box, mabeki waliteseka, kipa akapata taabu na mashabiki wakazibwa midomo mtaani.

Alianza kutengeneza ufalme mitaa ya Manungu kwenye mashamba ya miwa na baadae akawa kipenzi cha wanaSimba. Uzuri wa mashabiki huwa na wewe kipindi cha furaha, ila ukitetereka hakuna mwenye haja na wewe. Shiza Kichuya anapitia njia hiyo hiyo iliyowamaliza wachezaji kibao.

Katoka Simba na kuhamia nchini Misri, na maisha yakamshinda huko na karudi tena Simba bado mambo hayajakaa sawa na kiti cha ufalme alichoacha kuna wengine washkikalia. Lazima apambane kuuwasha moto tena na ikiwezekana aondoke Simba, au achague kuendelea kukaa Simba na kukaa ubaoni kama kaka yake Ndemla.

Kufeli kwake Misri kunanikumbusha stori ya kaka yake mmoja ambaye ashawahi kutimkia nchini Sweden na akarudi. Alipoulizwa alisema maisha ya kule yalimshinda. Sio kwamba maisha yanawashinda hawa wachezaji wetu kwa namna tunavyofikiria sisi bali kuna mengi nyuma ya pazia. (Ntakuja kuwaeleza hapa siku moja). Ni njia hii iliyomtesa Shiza Misri na zitakazowatesa wengi.

Ubora wake alioondoka nao sio ule aliorudi nao. Dakika chache alizocheza zilionesha hakuwa vizuri kimwili kwa ajili ya mpira. Alionekana kuwa mzito na mchovu. Hapa ndipo Miquissone na Chama wanatake advantage na tunaishia kulalama kuwa wachezaji wetu hawapewi nafasi.

Leo hii Kichuya kapoteza hadi nafasi ya kukaa benchi pale Simba. Simba sio Ndanda kuwa itamsubiri Kichuya akae sawa. Simba sio Benfica kuwa wanafanya biashara ya wachezaji watamvumilia akuze kiwango chake. Wakiona anakula na kulala bure watamuacha, kuepuka fedheha hii lazima achague maisha nje ya Simba. Simba wanahitaji material iliyotiyari kwa ajili ya matumizi. Viongozi na mashabiki wanahitaji kuendelea kutamba mtaani ila sio kukuza ubora wa Kichuya tena. Wanahitaji Chama, Kichuya, Bocco na Kagere walio tiyari kuwapa burudani ndani na nje ua uwanja.

Wakati haumsubiri Kichuya, lazima aangalie namna ya kucheza na sarafu vizuri.
Me sijui ni nani atauwasha moto wa Kichuya tena. Nasubiri nione.

Kwa maoni na Ushauri usisahau Kunitumia Sms 0676603330.
 
Kichuya alifanya kosa kurudi simba kwenye dirisha dogo! Bora angerudi Mtibwa ambao wako vizuri kunoa vipaji vilivyofifia! Ila haka kajamaa wacha tu kapotee, kalitutesa sana miaka ile na vigoli vyake vya ' kichawi'!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo njaaa jamanii,hapo Simba hata km haichezi lakini anauhakika na kula. Usishangae akawa anaingiza Mil.4 kwa mwezi.

Sawa, atalipwa msimu mmoja kisha anatemwa! Bora angeenda Manungu ambako angelipwa pesa ya kawaida na angenoa kipaji chake upya! Dilunga alipotea katika soka, alivyoenda Manungu akawa mpya!

Miraji alionekana kaisha, akaenda Lipuli akawa wa moto balaa! Yusufu Mhilu alipotea pale Yanga, sasa yupo Kagera katika kiwango cha juu sana! Hata Pato na Kaheza wameenda Polisi na sasa wapo vizuri sana! Kichuya toka Simba tafuta timu urudishe kiwango chako!

CC Hamis Said Ndemla
 
Aende mtibwa au kagera hapo simba hana chake timu ina mafundi wengi
 
Haya yote yanawahusu Ajibu Gadiel Kakulanya utafikiri wamebandikwa gundi kukalia Simba bila kucheza karinu msimu mzima hasa Gadiel na Ajibu walikimbilia Simba bila kujua kuwa wanafuata benchi hata ungelipwa m4 ni bora uende mahali utakapolipwa pungufu na watu wanakuona hata timu za nje zinakuona Nani atasajili mkalia benchi hasa timu za nje
 
Unakuta uongozi unabishana na benchi la ufundi, Kichuya abaki kichuya tumuache. Ni sawa na Ndemla, Mlipili, Rashid Juma, Alli Salim.

"Not everything is for everybody"
 
Kosa kubwa alilolifanya ni kubweteka baada ya kurudi toka Misri.

Hapa ndipo unapoona wachezaji wetu kukosa malezi ya soka.
Vilevile viongozi wetu kukosa utaalam wa soka.

Kichuya alianza kujikataa mwenyewe kula mawali maharage na michemsho hovyohovyo katoka kabisa kwenye soka.

Kiongozi unamsajili wa nn? Mchezaji mpitishe kwa wanaohusika na utaalamu wa afya za wachezaji watatoa ripoti, akafanye moja mbili ,tatu baada ya miezi kadhaa atakuwa fit kuitumikia klabu.

Unapiga hesabu , tunamsajili kwa mkataba wa miezi 6 ili awe fit anahitaji miezi mitatu kwa program maalum hivyo anabakiwa na miezi mitatu ya kuitumikia klabu.

Hapa kwa hadhi ya timu yetu, ss hatusubiri mchezaji HAKUNA nafasi.
Lkn ile parcent tutaipataje? Mhhhh mpe mkataba huyu si ndo anawafungaga yanga!!!! Unashangaa uwekezaji wote bado tupo "shehe yuleyule, kanzu ndo mpya"

Kwangu mm KICHUYA, anatakiwa aishi kimpira maana soka kwa mchezaji ni mateso kwa kuwa ni kazi fanya kazi muda wote ondoa likitambi lako.
 
Katika ulimwengu wa burudani hususani katika soka kuna wachezaji watoa burudani na wachezaji wa mpira. Pia kuna wale wanaokupatia vyote viwili kwa wakati mmoja.

Pia katika soka kuna wale wachezaji hupenda kutumia mguu wa kushoto. Kule ulaya kuna wachezaji tunawahusudu kama Messi, Alba, Ozil, Alaba na wengineo wengi. Vipi hapa bongoland, nani asiyemjua Shiza Kichuya, Zimbwe Jr., Miquisson na wengineo wengi. Hawa watu wapo very talented!

Raha ya wachezaji wa namna hii ni kuwa akiwa anaujua mpira, anakuonesha kuwa kweli mpira ni kazi yake.

Pale Simba kuna Shiza Ramadhan Kichuya, Mluguru fulani hivi mwenye kimo cha kupanda minazi. Guu lake la kushoto limetengenezwa kwa ajili ya kuwaadhibu mabeki, kuwatesa viungo na kuwamaliza makipa. Yanga wanamkumbuka vizuri mwaka 2017 mchezo wa round ya pili na goli lake la nje ya box, mabeki waliteseka, kipa akapata taabu na mashabiki wakazibwa midomo mtaani.

Alianza kutengeneza ufalme mitaa ya Manungu kwenye mashamba ya miwa na baadae akawa kipenzi cha wanaSimba. Uzuri wa mashabiki huwa na wewe kipindi cha furaha, ila ukitetereka hakuna mwenye haja na wewe. Shiza Kichuya anapitia njia hiyo hiyo iliyowamaliza wachezaji kibao.

Katoka Simba na kuhamia nchini Misri, na maisha yakamshinda huko na karudi tena Simba bado mambo hayajakaa sawa na kiti cha ufalme alichoacha kuna wengine washkikalia. Lazima apambane kuuwasha moto tena na ikiwezekana aondoke Simba, au achague kuendelea kukaa Simba na kukaa ubaoni kama kaka yake Ndemla.

Kufeli kwake Misri kunanikumbusha stori ya kaka yake mmoja ambaye ashawahi kutimkia nchini Sweden na akarudi. Alipoulizwa alisema maisha ya kule yalimshinda. Sio kwamba maisha yanawashinda hawa wachezaji wetu kwa namna tunavyofikiria sisi bali kuna mengi nyuma ya pazia. (Ntakuja kuwaeleza hapa siku moja). Ni njia hii iliyomtesa Shiza Misri na zitakazowatesa wengi.

Ubora wake alioondoka nao sio ule aliorudi nao. Dakika chache alizocheza zilionesha hakuwa vizuri kimwili kwa ajili ya mpira. Alionekana kuwa mzito na mchovu. Hapa ndipo Miquissone na Chama wanatake advantage na tunaishia kulalama kuwa wachezaji wetu hawapewi nafasi.

Leo hii Kichuya kapoteza hadi nafasi ya kukaa benchi pale Simba. Simba sio Ndanda kuwa itamsubiri Kichuya akae sawa. Simba sio Benfica kuwa wanafanya biashara ya wachezaji watamvumilia akuze kiwango chake. Wakiona anakula na kulala bure watamuacha, kuepuka fedheha hii lazima achague maisha nje ya Simba. Simba wanahitaji material iliyotiyari kwa ajili ya matumizi. Viongozi na mashabiki wanahitaji kuendelea kutamba mtaani ila sio kukuza ubora wa Kichuya tena. Wanahitaji Chama, Kichuya, Bocco na Kagere walio tiyari kuwapa burudani ndani na nje ua uwanja.

Wakati haumsubiri Kichuya, lazima aangalie namna ya kucheza na sarafu vizuri.
Me sijui ni nani atauwasha moto wa Kichuya tena. Nasubiri nione.

Kwa maoni na Ushauri usisahau Kunitumia Sms 0676603330.
Duuh! Umetumia busara kubwa sana kumwambia Star asiye jitambua kuwa yeye amepitwa na wakati na ni mda mwafaka achukue maamuzi ya kuiacha simba na kutafuta riziki nyingine nje ya simba.

Ni kweli kwamba sisi waafrika wengi tunapenda sana kung'ang'ania vitu ambavyo vimekwisha tupungia mikono tayari na kutuambia bye bye. Kisa cha kufanya hivyo ni kwamba wengi wetu tuna dumaa na na sifa za kale.

Lakini hata hivyo tujirizishe sisi qenyew pia kuwa hata wenzetu wa nchi za kwanza wanamatatizo hayo hayo. Ukiona mtu au nchi inafanya mambo ya yafuatayo; ukimya mwingi na ubabe inapobidi ujue bye bye iko hewani.

Hicho ndicho kilicho mpata huyo mchezaji uliye jaribu kumtahadharisha mwenendo wake. Nilikuwa simjui lakini kwa kuchukua maelezo ya uchambuzi wako kama ni ya kweli basi sinabudi kumweleza ndugu yetu aanze kuchukua hatua za kujijengea maisha bila simba au nje ya simba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom