Ayenda M
Member
- Jan 4, 2018
- 98
- 132
Katika ulimwengu wa burudani hususani katika soka kuna wachezaji watoa burudani na wachezaji wa mpira. Pia kuna wale wanaokupatia vyote viwili kwa wakati mmoja.
Pia katika soka kuna wale wachezaji hupenda kutumia mguu wa kushoto. Kule ulaya kuna wachezaji tunawahusudu kama Messi, Alba, Ozil, Alaba na wengineo wengi. Vipi hapa bongoland, nani asiyemjua Shiza Kichuya, Zimbwe Jr., Miquisson na wengineo wengi. Hawa watu wapo very talented!
Raha ya wachezaji wa namna hii ni kuwa akiwa anaujua mpira, anakuonesha kuwa kweli mpira ni kazi yake.
Pale Simba kuna Shiza Ramadhan Kichuya, Mluguru fulani hivi mwenye kimo cha kupanda minazi. Guu lake la kushoto limetengenezwa kwa ajili ya kuwaadhibu mabeki, kuwatesa viungo na kuwamaliza makipa. Yanga wanamkumbuka vizuri mwaka 2017 mchezo wa round ya pili na goli lake la nje ya box, mabeki waliteseka, kipa akapata taabu na mashabiki wakazibwa midomo mtaani.
Alianza kutengeneza ufalme mitaa ya Manungu kwenye mashamba ya miwa na baadae akawa kipenzi cha wanaSimba. Uzuri wa mashabiki huwa na wewe kipindi cha furaha, ila ukitetereka hakuna mwenye haja na wewe. Shiza Kichuya anapitia njia hiyo hiyo iliyowamaliza wachezaji kibao.
Katoka Simba na kuhamia nchini Misri, na maisha yakamshinda huko na karudi tena Simba bado mambo hayajakaa sawa na kiti cha ufalme alichoacha kuna wengine washkikalia. Lazima apambane kuuwasha moto tena na ikiwezekana aondoke Simba, au achague kuendelea kukaa Simba na kukaa ubaoni kama kaka yake Ndemla.
Kufeli kwake Misri kunanikumbusha stori ya kaka yake mmoja ambaye ashawahi kutimkia nchini Sweden na akarudi. Alipoulizwa alisema maisha ya kule yalimshinda. Sio kwamba maisha yanawashinda hawa wachezaji wetu kwa namna tunavyofikiria sisi bali kuna mengi nyuma ya pazia. (Ntakuja kuwaeleza hapa siku moja). Ni njia hii iliyomtesa Shiza Misri na zitakazowatesa wengi.
Ubora wake alioondoka nao sio ule aliorudi nao. Dakika chache alizocheza zilionesha hakuwa vizuri kimwili kwa ajili ya mpira. Alionekana kuwa mzito na mchovu. Hapa ndipo Miquissone na Chama wanatake advantage na tunaishia kulalama kuwa wachezaji wetu hawapewi nafasi.
Leo hii Kichuya kapoteza hadi nafasi ya kukaa benchi pale Simba. Simba sio Ndanda kuwa itamsubiri Kichuya akae sawa. Simba sio Benfica kuwa wanafanya biashara ya wachezaji watamvumilia akuze kiwango chake. Wakiona anakula na kulala bure watamuacha, kuepuka fedheha hii lazima achague maisha nje ya Simba. Simba wanahitaji material iliyotiyari kwa ajili ya matumizi. Viongozi na mashabiki wanahitaji kuendelea kutamba mtaani ila sio kukuza ubora wa Kichuya tena. Wanahitaji Chama, Kichuya, Bocco na Kagere walio tiyari kuwapa burudani ndani na nje ua uwanja.
Wakati haumsubiri Kichuya, lazima aangalie namna ya kucheza na sarafu vizuri.
Me sijui ni nani atauwasha moto wa Kichuya tena. Nasubiri nione.
Kwa maoni na Ushauri usisahau Kunitumia Sms 0676603330.